Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Mamlaka za Udhibiti kwenye Uandaaji Taarifa za Fedha kwa mwaka 2024, katika tuzo zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu Tanzania (NBAA).
Tuzo hiyo ilikabidhiwa tarehe 4 Disemba 2025, ikitambua ubora wa TCAA katika uwazi, usahihi na uzingatiaji wa viwango vya kimataifa vya uhasibu. Huu ni ushindi mkubwa ikizingatiwa kuwa mwaka uliopita Novemba 2024 TCAA ilishika nafasi ya 3 katika Uandaaji Taarifa za Fedha kwa mwaka 2023.
TCAA ikiongozwa Na Mkurugenzi Mkuu Salim Msangi wanasema tuzo hiyo inaakisi maboresho makubwa yaliyofanywa katika mifumo ya usimamizi wa fedha, uandaaji wa taarifa na uwajibikaji.
Tuzo hizo za NBAA zinalenga kuhamasisha viwango bora vya uandaaji wa taarifa za fedha. Safari ya TCAA kutoka nafasi ya 3 mwaka 2023 hadi nafasi ya 1 mwaka 2024 inaonesha dhamira ya dhati ya kuboresha utendaji na kuongoza katika sekta ya udhibiti wa anga nchini.
Aidha, tuzo hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb.) ambaye alimwakilisha Waziri wa Fedha katika ufungaji wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo.
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Dastan Nkanabo alipokea tuzo kwa niaba ya Mamlaka.
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb) (kulia) akikabidhi tuzo mshindi wa kwanza katika kundi la Mamlaka za Udhibiti kwa Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Dastan Nkanabokatika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2024 (Best Presented Financial Statements for the Year 2024 Awards) zinayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA).
Picha ya pamoja





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...