NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
CHUO Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) kipo katika mchakato wa kuboresha sera na mikakati yake ili kuendana na kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani, ikiwemo mapinduzi ya akili-mnemba (AI) na matumizi ya kidijitali katika ujifunzaji, ufundishaji na utafiti.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika Mahafali ya 55 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar, amesema mageuzi hayo yanakwenda sambamba na ujenzi wa miundombinu ya kisasa ili kuimarisha mazingira wezeshi ya kiteknolojia na kuongeza ubora wa elimu na tafiti bunifu.
“Chuo kimepitia upya mitaala yake ili kuimarisha ujifunzaji unaojikita katika ubunifu na ujasiriamali (entrepreneurship-based learning),” amesema Balozi Maajar.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Anangisye, amesema UDSM imewezesha utambuzi wa zaidi ya bunifu 120 pamoja na usajili wa kampuni changa 39, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukuza ubunifu na ujasiriamali miongoni mwa wanafunzi na wahadhiri.
Aidha, amesema chuo kimetoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanafunzi 569, wakiwemo wanafunzi 65 wenye ulemavu, hatua ambayo inasisitiza kujenga uwezo jumuishi kwa maendeleo endelevu.
Akizungumzia utekelezaji wa Mradi wa HEET, Prof. Anangisye amesema ujenzi wa zaidi ya majengo 21 mapya ya kisasa na ukarabati wa majengo 3 kwa ajili ya kufundishia na ofisi za wahadhiri umefikia asilimia 75.
Majengo hayo yanajengwa katika Kampasi ya Dar es Salaam, Taasisi ya Sayansi za Bahari Zanzibar (IMS), Kampasi ya Kagera, na Kampasi ya Lindi.
Katika kuimarisha uwezo wa kitaaluma, Prof. Anangisye amesema chuo kimefadhili masomo ya wanataaluma 29 katika Shahada ya Uzamivu (PhD) kwenye vyuo vikuu bora duniani, ambapo 12 kati yao (25%) ni wanawake.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...