Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kilosa wamempitisha Diwani wa Kata ya Mtumbatu, Mhe. Aman Sewando kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri katika uchaguzi uliofanyika leo Disemba Mosi 2025
Sewando ambaye amekuwa akitumikia wananchi wa Mtumbatu kama diwani ameibuka kidedea kwa kupata kura 29 huku anaye mfuata alipata kura 22.
Akitoa neno la shukurani baada ya kutangazwa mshindi, Mhe. Sewando aliwashukuru madiwani kwa kumuamini na kumkabidhi jukumu hilo, akiahidi kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuharakisha maendeleo ya wilaya ya Kilosa
“Nawashukuru sana madiwani wenzangu kwa imani waliyoonyesha. Huu ni uongozi wa ushirikiano; tutaweka mbele maslahi ya wananchi wa Kilosa na kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi,” alisema Sewando.
Baadhi ya wana CCM na wananchi wa Kilosa wamepokea taarifa za uchaguzi huo kwa matumaini, wakisema kuwa Diwani huyo amekuwa mstari wa mbele kushirikiana na jamii na kusimamia vyema miradi ya huduma za jamii katika Kata ya Mtumbatu.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...