Vijana wa Kitanzania maarufu kizazi cha Gen Z, wameshauriwa kuzingatia misingi ya Amani, na utulivu, sambamba na kutii sheria za nchi katika kuelekea maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika Desemba 9 mwaka huu.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 3,2025 Jijini Dar es Salaam.
Msama ametumia nafasi hiyo kuwaeleza Vijana kuwa wana wajibu wa kutambua amani ni nguzo muhimu katika Taifa, na kwamba wasikubali kutumika na watu wenye nia ovu na nchi yao, badala yake wanapaswa kuwa wa kwanza kuilinda amani iliyopo kwa namna yoyote
Amesema wazazi wana wajibu wa kuwakanya na kuwaonya watoto wao,kuhakikisha hawashiriki ama kukumbwa na misukumo isiyokuwa na tija.
Katika hatua nyingine, Msama amewasihi viongozi wa dini kuendelea kutoa na kuesambaza elimu ya kutetea amani na vijana kusikiliza maelekezo yao.
Msama amebainisha kuwa hata wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wanapaswa kuendelea kuhimiza vijana kuheshimu sheria za nchi, kwani hakuna haki inayoweza kutetewa nje ya misingi ya sheria na amani.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...