Halmashauri ya wilaya ya Geita imepokea zana za kilimo kutoka wizara ya kilimo ikiwa ni mkakati wa kuendelea kuwawezesha wakulima katika halmashauri hiyo kufanya kazi kwa urahisi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Dkt Alphonce Bagambabyaki ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kutoa zana hizo kuwasaidia wakulima katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imetoa trekta 5 na Pawatila 16 pamoja na viambata vyake hii ikitarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa wakulima.
" Tunashukuru Serikali kwa kutupatia zana hizi kwani Uhitaji ni mkubwa sana kwani shughuli za Kilimo hususani zao la Mpunga zinafanyika kwa kiasi kikubwa katika maeneo yetu" Amesema Dkt Alphonce.
Vile Vile Dkt Alphonce amesema zana hizo zitawasaidia wakulima wakubwa na wadogo na kwa kuzingatia jiografia ya Maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita Pawatila zitatumika kwa maeneo ambayo Trekta hazitaweza kufika na kwa wakulima ambao hulima ekari chache.
Pamoja na hayo Kaimu Mkurugenzi amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Geita Mhe Joseph Kasheku Musukuma kwa juhudi zake katika upatikanaji wa zana hizo ambazo zitaenda kuongeza uzalishaji ndani ya Halmashauri na kukuza uchumi wa wananchi.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...