JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linapenda kujulisha kuwa limemkamata na linamshikilia Award Karonga, Mkazi wa Katumba ambaye ni Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] Wilaya ya Rungwe na pia ni Makamu Mwenyekiti Hamasa Taifa wa chama hicho.
Alikamatwa Januari 29, 2026 saa 4 asubuhi maeneo ya Mtaa wa Katumba, Kata ya Ibighi - Tukuyu Wilaya ya Rungwe kwa tuhuma mbalimbali za kijinai ikiwepo uchochezi.
Upelelezi unakamilishwa ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...