Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb) ameelekeza mambo sita muhimu kuzingatia ili ushirika kuimarika zaidi na kuleta tija kwa wanaushirika.
Akizungumza tarehe 30 Januari 2026 jijini Dodoma wakati akizindua Bodi ya Makamishna wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Waziri Chongolo amesema Kamisheni ihakikishe inaleta mageuzi ya kidigitali ili takwimu sahihi zipatikane kwenye mizani ya kidigitali na kupunguza udanganyifu kwa wanachama na wakulima.
Jambo la pili ameielekeza Kamisheni kuhakikisha ukaguzi unafanyika kwa vyama vyote vya ushirika nchini kila mwaka na hatua stahiki kuchukuliwa kwa wahusika wote wanaokiuka taratibu na kurudisha nyuma jitihada za maendeleo ya ushirika. Pia, masoko ya nje yatafutwe ili bidhaa zinazozalishwa na Vyama vya Ushirika ziuzwe na kuleta tija ya mitaji.
Kuhusu suala la nne, Kamisheni imetakiwa kuhakikisha mali za vyama vya ushirika zinawekezwa ipasavyo ili ziweze kuzalisha na kusaidia kuleta maendeleo yanayotarajiwa na wanaushirika. Sambamba na hilo, uadilifu, weledi na ubunifu vimetiliwa mkazo kuwa ni chachu ya kuimarisha ushirika.
Aidha, jambo la mwisho ni kuhakikisha kunakuwa na ujenzi wa viwanda, upatikanaji wa huduma za bima ya mazao, huduma za matibabu na mafao ya uzeeni kwa wakulima.
“Ni matumaini yangu kuwa Kamisheni hii itaweza kutekeleza haya kwa weledi na niwapongeze tena Wajumbe wote kwa kuteuliwa kwani tunahitaji kuleta matokeo kwa wakulima,” amesema Mhe. Chongolo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Bw. Abdulmajid Nsekela amemuhakikishia Mhe. Waziri Chongolo kuwa Bodi na pia kwa kushirikiana na Mrajis na Mtendaji Mkuu wa lTCDC, Dkt Benson Ndiege watatekeleza maelekezo yake katika kuhakikisha ushirika unakuwa nguzo ya uchumi shirikishi utakaochochea ajira na maendeleo ya Taifa.



.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...