Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah amekutana na kuzungumza na Balozi wa Urusi nchini Mhe. Andrey Avetisyan aliyemtembelea Ofisini kwake Zanzibar kwa ziara ya kikazi tarehe 26 Januari ,2026.
Viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa uwili na kutilia mkazo kuimarisha Utalii, Nishati, Elimu na Utamaduni na uhusiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya Tanzania na Urusi.
Katika mazungumzo hayo Mhe. Hemed Suleiman Abdullah amesisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iko tayari kuhakikisha mazingira wezeshi kwa wawekezaji kutoka Urusi wanaokwenda kuwekeza visiwani Zanzibar.
Naye Balozi Avetisyan ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa utayari wake wa kuimarisha biashara na uwekezaji kati ya Urusi na Tanzania.
Ametoa wito kwa SMZ kushiriki kikamilifu katika vikao vya Tume ya Pamoja ya Ushirikiano wa Kibiashara na Kiuchumi kati ya Urusi na Tanzania.
Awali Mhe. Balozi Avetisyan alikutana na kuzungumza na Kaimu Mkurungenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar Bw. Ali Suleyman Ali katika Ofisi hiyo.
Katika kikao hicho wamebadilishana mawazo kuhusu utekelezaji wa mipango ya pamoja na kukubaliana kuendelea na mashauriano kuhusu masuala ya ushirkiano wa uwili.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...