Katika jitihada za kuimarisha uchumi wa wananchi, Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) umethibitisha kuendeleza ushirikiano wa kimkakati na Serikali ya Tanzania katika kukuza sekta za uzalishaji hasa Kilimo na Uvuvi.
Leo, Januari 16, 2026, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dkt. Jim Yonazi, amefanya mazungumzo muhimu na Mkurugenzi Mkazi wa IFAD, Bw. Sakphouseth Meng, lengo likiwa ni kutathmini na kuendeleza miradi ya maendeleo nchini.
Katika kikao hicho, Bw. Meng ametoa habari njema kwa kusema kuwa IFAD itaendelea kutoa mikopo na rasilimali fedha kwa ajili ya miradi itakayowanufaisha wakulima na wavuvi.
Maeneo aliyoyagusia Mkurugenzi Mkazi huyo ni Kukuza uchumi wa watu wa vijijini, Kuongeza tija katika sekta ya Kilimo na Uvuvi, Kusaidia wananchi kujikwamua kiuchumi kupitia miradi ya maendeleo kwenye sekta hiyo.
Kwa upande wake, Dkt. Jim Yonazi ameuhakikishia uongozi wa IFAD kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo tayari wakati wote kushirikiana nao. Amebainisha kuwa hatua kubwa imepigwa hadi sasa na ushirikiano huo umekuwa na tija ya moja kwa moja kwa Mtanzania wa hali ya chini
"Serikali ipo tayari kuendeleza ushirikiano huu kwani mafanikio yaliyoonekana ni makubwa na yanagusa maisha ya watu wetu," alisema Dkt. Yonazi.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na wataalamu na viongozi waandamizi, akiwemo Dkt. Jacqueline Motcho – Afisa Programu Mkazi wa IFAD, Bw. Paul Sangawe -Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu (OWM), Bw. Salum Mwinjaka – Mratibu wa Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP).
Kuendelea kwa ushirikiano huu ni ishara tosha ya kuimarika kwa Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), ambayo imekuwa mhimili mkuu katika kusaidia sekta hizo nchini Tanzania.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...