Na MWANDISHI WETU

MEYA wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Nurdin Bilal ‘Sheta’ amefungua rasmi Ofisi ya Diwani Kata ya Kisutu Tousif Mohammedali Bhojani na kumtaka diwani huyo kukaa ofisini kusikiliza na kutatua kero za wananchi badala ya kumweka mwakilishi.

Sheta ameifungua Ofisi hiyo leo baada ya ukarabati mkubwa uliofanywa na Diwani Bhojani wenye lengo la kuandaa mazingira bora ya kuwahudumia wananchi.

“Usiweke mwakilishi wa kusikiliza kero za wananchi. Kaa wewe ofisini uwasikilize. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anatutaka tusikilize na kutatua kero za wananchi wetu. Huu ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Wananchi wa Kata ya Kisutu njooni katika ofisi yenu hii na kero zenu zitatatuliwa na zikishindikana leteni katika ofisi yangu,”amesema Sheta.

Diwani Bhojani amesema lengo la kukarabati ofisi hiyo ni kutekeleza ahadi aliyoitoa ya kuifanya kuijenga Kisutu Mpya, inayo tatua na kusikiliza kero za wananchi.

“Katika ofisi hii nitakuwepo Jumatano na Alhamisi kusikiliza na kutatua kero za wananchi. Wananchi wa Kisutu walikuwa na shida kwa sababu hawakujua ni wapi wanapeleka shida zao ngazi ya kata. Sasa ofisi ipo na tumeiboresha. Waje tutawahudumia vizuri,”ameeleza Bhojani.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Said Sidde, alipongeza hatua ya Diwani Bhojani kukarabati ofisi hiyo na kuwataka wananchi kuitumia kwani Chama kimetoa maelekezo kwa madiwani , watendaji na watumishi wa serikali kuhakikisha wanawasikiliza wananchi na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zao.

Baadhi ya wananchi wa kata hiyo wamesema nuru njema imeanza kuonekana tangu diwani huyo aingie madarakani kwani amekuwa karibu na wananchi hivyo imekuwa ni rahisi kusikilizwa kero zao.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...