Shirika la Masoko ya Kariakoo, katika kuimarisha shughuli za zimamoto na ukoaji katika maeneo ya Kariakoo limelipatia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kizimamoto Ilala Ofisi na eneo la kuegesha gari lao kwa ajili ya shughuli zao ili kupunguza usumbufu kwa wananchi wa maeneo hayo wakati majanga ya moto yanapojitokeza.
Hayo yamesemwa na Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo CPA. Ashraph Abdulkarim alipokutana na uongozi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kizimamoto Ilala kwa lengo la kujadiliana maeneo mbalimbali ya kushirikiana baina ya taasisi hizo mbili.
CPA. Abdulkarim ameongeza kuwa ushurikiano baina ya taasisi hizo ni muhumu kwa kuwa utawezesha Soko la Kariakoo na jamii inayozunguka soko hilo kuwa salama, na kufanya biashara bila wasiwasi wowote na kuendelea kuchangia uchumi wa taifa.
Kwa upande wake Kamanda za Zimamoto na Ukoaji Mkoa wa Kizimamoto Ilala, SACP. Peter Mabusi amesema Jeshi hilo litashirikiana na Shirika la Masoko ya Kariakoo kwa kutoa kutoa elimu kwa wafanyabiashara na watumishi wa shirika, kufanya ukaguzi wa mifumo ya kuzima moto ili kuwezesha kukabiliana na majanga kadiri yatakavyojitokeza.
Ikumbukwe kuwa Shirika la Masoko ya Kariakoo limekuwa likitoa mchango wa maji kutoka katika visima vilivyopo Soko la Kariakoo ambapo mpaka sasa limeshatoa Zaidi ya lita za ujazo 134,800 ambazo zimetumika kudhibiti matukio ya ajali za moto katika maeneo ya Kariakoo kwa kipindi cha mwezi Septemba 2025 hadi sasa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...