MERIDIANBET imeendelea kuthibitisha kuwa mchango wake hauishii kwenye burudani ya michezo ya kubashiri pekee, bali unagusa moja kwa moja maisha ya wananchi. Kupitia mkakati wake wa uwajibikaji kwa jamii (CSR), kampuni hiyo imeshiriki kikamilifu katika zoezi la usafi wa mazingira Kata ya Mbezi Juu, ikionesha dhamira ya kweli ya kushiriki maendeleo ya kijamii na kiafya ya wananchi.
Katika kuimarisha mapambano dhidi ya
uchafu na magonjwa yanayotokana na mazingira yasiyo safi, Meridianbet
ilishiriki usafi pamoja na kukabidhi vifaa mbalimbali vya usafi ikiwemo mifagio
imara, mafyekeo, koleo, glovu, mifuko
ya taka pamoja na viatu maalum vya kazi. Msaada huu ulilenga kuendeleza zoezi
la usafi kwa muda mrefu na kwa ufanisi zaidi.
Akizungumza kwa niaba ya kampuni,
mwakilishi wa Meridianbet Nancy Ingram alieleza kuwa mazingira safi ni
nguzo muhimu ya kuzuia magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, homa ya matumbo
na maambukizi mengine yanayohusiana na uchafu. Alisisitiza kuwa Meridianbet inaamini
kuwa jamii yenye afya bora ndiyo msingi wa maendeleo ya kweli.
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna
michezo mbalimbali ya kasino
mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri
zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku.
Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga
*149*10#.
Diwani wa Kata ya Mbezi Juu
aliipongeza Meridianbet kwa kuonesha ushirikiano wa dhati na serikali za
mitaa katika kulinda mazingira. Alieleza kuwa mchango wa sekta binafsi katika
shughuli za kijamii ni kichocheo muhimu cha uwajibikaji wa pamoja, kwani
huongeza hamasa kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda afya zao na
mazingira yanayowazunguka.
Kupitia tukio hili, Meridianbet
imeweka wazi kuwa itaendelea kuwekeza katika miradi ya kijamii yenye athari
chanya kwa maisha ya wananchi. Kampuni hiyo
imesisitiza kuwa usafi wa mazingira ni wajibu wa kila mdau, na itaendelea
kushirikiana na jamii, viongozi na taasisi mbalimbali kuhakikisha
mazingira yanabaki kuwa salama.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...