Na Seif Mangwangi, Michuzi TV Arusha
WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA), imeingia rasmi makubaliano na chuo cha ufundi Arusha (ATC), ya kutengeneza mita janja za maji zitakazokuwa zikitumika kwa malipo ya maji ya kabla.
Akizungumza katika zoezi la kutia sahihi makubaliano hayo lililofanyika leo 16 Januari 2026 katika chuo cha ufundi Arusha (ATC), Mkurugenzi Mkuu wa Ruwasa, Mhandisi Walter Kirita, amesema dira hizo zinaenda kumaliza malalamiko mengi ya wananchi kubambikiwa bili za maji.
Aidha amesema tatizo la upotevu wa mapato yanayotokana na matumizi yasiyosahihi ya maji pia yanaenda kukomeshwa kupitia ujio wa mita hizo janja.
Amesema tayari majaribio ya mita janja 100 zilizotengenezwa na chuo cha ufundi Arusha (ATC), zimefungwa katika maeneo mbalimbali ya taasisi za umma na watu binafsi na yameonyesha kufanya vizuri.
“ Baada ya malalamiko ya wananchi kwenye bili za maji tulifanya utafiti na kuamua kutengeneza mita janja za majaribio ambapo Juni 2022 tuliwapa wenzetu wa ATC kazi hii na ambao Kwa kweli walifanya vizuri sana na sasa tunaenda kuwapa kazi hii,”amesema.
Amesema kwa kuanzia Ruwasa inahitaji zaidi ya mita janja laki tatu na elfu hamsini (350,000), kupitia vyanzo vya maji 5000 vilivyopo chini ya mamlaka hiyo kote nchini.
Mkuu wa chuo cha ufundi Arusha Profesa Musa Chacha amesema chuo hicho kupitia kampuni yake tangu ya ATC PLC imejipanga kutengeneza mita hizo kwa ubora wa hali ya juu na kuondoa malalamiko ya wananchi ya kubambikiwa maji.
Amesema makubaliano hayo ni muendelezo wa ushirikiano kati ya chuo hicho na taasisi mbalimbali za umma na binafsi kutokana na ubunifu ambao umekuwa ukifanywa na walimu pamoja na wanafunzi chuoni hapo.
“ ATC tumejipanga kukamilisha kazi hii kadiri mteja wetu atakavyotaka, tuna wataalam wa kutosha sana kupitia kiwanda kilichopo hapa hapa chuoni, sisi tunatumia viwanda hivi kufundishia wanafunzi wetu lakini pia kuzalisha bidhaa mbalimbali, ni kama kule Kikuletwa, tumejenga mtambo wa kuzalisha umeme lakini ndio huo huo utatumika kufundishia wanafunzi wetu mambo ya Nishati,”amesema.
Awali Kaimu Meneja huduma za ufundi kutoka Ruwasa Mhandisi Davis Rweyemam amesema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka Jana 2025, Ruwasa ilikuwa imeshaunganishia huduma ya maji taasisi na watu binafsi 347435 kati yake vituo 147905 ni vituo vya umma na 199530 ni watu binafsi.
“ Kati ya idadi ya waliounganishiwa maji asilimia 69.6 wanatumia dira za maji na kati yao asilimia 99.5 wanatumia dira za maji za baada, hii imeleta malalamiko mengi sana na sasa tumekuja na mfumo huu wa dira ya maji ya kabla,” amesema.
Mkurugenzi wa kampuni tanzu ya chuo cha ufundi Arusha ATC Plc, Mhandisi Faraji Magania amesema tangu kuanzisha kwa kampuni hiyo tenda nyingi za ujenzi na usanifu wa majengo wamekuwa wakipewa kwa kuwa wamekuwa wakitumia gharama nafuu zaidi.
Amesema kampuni hiyo imeshafanya usanifu wa majengo mbalimbali pamoja na ujenzi wake ikiwemo ujenzi wa weni na ukumbi wa mihadhara katika chuo cha TICD Tengeru, vyuo 63 vya Ualimu nchini chini ya wizara ya elimu Sayansi na teknolojia, na ujenzi wa bweni na madarasa na zahanati katika chuo cha utalii Kampasi ya Arusha.
Magania amesema kwa mwaka kampuni hiyo imekuwa ikiingiza mapato ya zaidi ya Bilioni2, na kwamba kutoka na kuendeleza kuaminifu mapato hayo yataendelea kupanda.
Serikali chini ya utawala wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ilishaagiza kuondolewa Kwa dira za maji zinazotumika hivi sasa za malipo ya maji baada Kwa kuwa zimekuwa zikileta malalamiko mengi kutoka Kwa wananchi ikiwemo kubambikiwa bili za maji.

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...