Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imewakamata watuhumiwa 66 akiwepo raia wa Kenya aliyekamatwa akiwa na dawa za kulevya aina ya heroin gramu 131.88.
Akizungumza leo Januari 8,2026 jijini Dar es Salaam Kamishina Jeneral Aretas Lyimo amesema katika operesheni iliyofanyika Sinza C mtaa wa Bustani numba namba 16, Jefferson Kilonzo Mwende (35), raia wa Kenya, alikamatwa akiwa na gramu 131.88 za heroin.
Amesema mtuhumiwa huyo aliyeishi Tanzania tangu 2023, alitumia biashara ya kuuza chai kuficha biashara ya dawa za kulevya anayoifanya.
“Mtuhumiwa huyu kwa sasa tunamshikilia kwa mahojiano zaidi na nitoe rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Mamlaka kutoa taarifa pale wanapomtilia shaka mtu yeyote.Niwahakikishie wote ambao wanajihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya tutawakamata na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.”
Wakati huo huo amesema katika eneo la Kinyerezi, mtaa wa Majoka wilaya ya Ilala, watuhumiwa Erick Ernest Ndagwa (32), Paul Blass Henry (34), na Tido Emmanuel Mkude (35) walikamatwa wakiwa na bangi kg 193.66, zikisafirishwa kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam.
Aidha amesema kutokana na ukaguzi uliofanyika kwenye kampuni za usafirishaji wa mizigo jijini Dar es Salaam, paketi 20 za dawa za kulevya aina ya mirungi zenye uzito wa kilogramu 9.54 zilikamatwa zikiwa zimefungwa kama majani ya mwarobaini yaliyokaushwa.
Amesema dawa hizo zilikuwa zikisafirishwa kutoka Kenya kuelekea Australia.Vilevile, kupitia operesheni mbalimbali zilifanyika katika mikoa ya Mwanza, Sinyanga, Morogoro, Tanga, Lindi, Kilimanjaro, Njombe, Kigoma na Arusha zilikamatwa dawa za kulevya aina ya heroin gramu 37.34, skanka kilogramu 1.015, bangi kilogramu 7,969.98 na mirungi kilogramu 1,363.701 pamoja na kuteketeza ekari 14 za mashamba ya bangi.
“Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inasisitiza wananchi kutoa taarifa kuhusu viashiria vya biashara ya dawa za kulevya na kuwa makini kutokubali kusafirisha mizigo wasiyoijua. Mamlaka itaendelea na operesheni nchi nima na kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wahalifu wa dawa za kulevya.”

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...