Na Mwandishi Wetu,Arusha.
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-Utumishi, Regina Qwaray,amewataka wananchi wa Wilaya ya Arumeru walionufaika na miradi iliyojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jami (TASAF), kuilinda kwa wivu mkubwa miradi hiyo ili idumu kwa muda mrefu na kuwapa huduma nnafuu.
Ametoa raia hiyo jana alipotembelea miradi ya mfereji wa umwagiliaji maji katika Kata ya Ngabobo uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Shule ya Sekondari Oldonyowas,iliyopo Halmashauri ya Arusha zote za wilayani Arumeru.
Akizungumza shuleni hapo amesema TASAF imepeleka miradi mikubwa ambapo shule hiyo ni miongoni mwa wanufaika ambao wamepata miradi tisa shuleni hapo hivyo ni muhimu wakaitunza kwa sababu itakapoharibika gharama ya kutengeneza tena ingeweza kujenga miradi kama hiyo maeneo mengine.
“Miradi tuitunze kwa wivu mkubwa na niwapongeze kwa kuweka uzio kwani mlisema watu walikuwa wanavamia eneo hili,tuendelee kuelimisha jamii miradi inapoletewa kwenye maeneo yetu wanufaika wakubwa ni wananchi wenyewe,miradi iwe sehemu yao wanapoiharibu wajue wameharibu mali yao,”amesema.
Naibu huyo amesema kupitia miradi hiyo itawasaidia watoto wa kike wa jamii ya kifugaji ambao awali walikuwa wakiozeshwa mapema ila kwa sasa wamejengewa shule karibu na vijiji vyao huku kukiwa na mabweni pia.
“Viongozi wa kata tuendelee kuwajengea imani wananchi na kuwapa elimu ya kupeleka watoto wetu shule hasa watoto wa kike ambao jamii imekuwa na utamaduni wa kuwaozesha mapema ,tutumie fursa zilizopo kwenye maeneo yetu vizuri kwa maendeleo ya jamii yetu kwa ujumla,”
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Afisa Miradi wa TASAF, Agustino Ngude, amesema katika shule hiyo kumetekelezwa miradi tisa ikiwemo nyumba za walimu nne, maabara mbili,jengo la utawala,mabweni manne ya wavulana mawili na wasichana mawili na uzio wa shule na kuwa kwa sasa wanafunzi wanasoma katika mazingira salama.
Akizungumzia mradi wa maji amesema awali kabla ya mradi huo mfereji ulikuwa na changamoto ya kujaa tope na mchanga na kiwango kikubwa cha maji kilikuwa kinapotea njiani badala ya kuwafikia wakulima ila baada ya utekelezaji wa mradi adha hiyo imeondoka.
“Kabla ya miradi hii awali zipo kaya nyingi zilikuwa zinaitwa kaya lengwa kipato chake kilikuwa ch chini ni kaya zilizokuwa zinapokea ruzuku na zilikuwa zinamudu kuwahudumia watoto wao na baadaya mradi wa umwagiliaji kaya maskini zimeongeza kipato chake zimeshiriki katika kilimo na kuongeza mapato,”amesema.
Akiwasilisha taarifa ya mradi wa mrefeji wa umwagiliaji,Mratibu wa TASAF Wilaya ya Meru, amesema mradi huo unanufaisha wananchi 4,184 wa vijiji vitatu ambavyo ni Oltepes, Ngabobo na Tank na zaidi ya wakulima 851 wanatumia mfereji huo kwa ajili ya kilimo cha nyaya,vitunguu na mbogamboga.
Amesema kwa sasa mfereji huo wenye urefu wa kilomita 8.2 umegharimu zaidi ya Sh 401.7milioni huku kukiwa na vigawa maji 32 katika mrefeji wote na kuwa wananchi wameongeza uzalishaji huku mapato ya halmashauri yakiongezeka kutoka Sh 4.5milioni hadi kufikia Sh 15milioni kwa mwezi.
Awali Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Arusha, Kabula Sukwa, amesema Kijiji hicho kimepata miradi tisa iliyotokana na kuwepo kwa hamasa ya kuainisha changamoto zinazowakabili wananchi katika mazingira yao.
“Kipindi cha nyuma jamii hii haikuwa inathamini elimu ila kwa sasa wamehamasika na wanapeleka watoto shule na kwa kuona hilo waliamua ujenzi wa madarasa,mabweni na miradi mingine itekelezwe,mabinti kwa sasa hawakumbani na changamoto ya kukosa elimu na uzio unasaidia kuhakikisha usalama wa wanafunzi wakiwa shuleni,”amesema.
Mmoja wa wananchi hao, Anna Kitomari,amesema awali walikuwa wakikumbana na migogoro kutokana na shida ya maji ila baada ya kukamilika kwa mradi huo migogoro mingi ya kugombe amaji imeisha na sasa wanazalisha mazao mbalimbali ikiwemo nyanya,vitunguu,mahindi na mbogamboga na kuuza hivyo kujiongezea kipato.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...