Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kushirikiana kwa ukaribu na wadau mbalimbali wakiwemo Serikali, wafanyabiashara, wawekezaji, wajasiriamali, wafanyakazi, wakulima pamoja na makundi mengine ya kijamii, kwa lengo la kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa taifa kupitia utoaji wa huduma jumuishi na bunifu za kifedha zinazoendana na mahitaji halisi ya makundi ya kiuchumi.

Hatua hiyo inalenga kuunga mkono jitihada za Serikali katika kujenga uchumi shindani na jumuishi, kwa kuhakikisha wananchi na taasisi mbalimbali wanapata huduma bora, nafuu na rafiki za kifedha zitakazowawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji na maendeleo.

 

Dhamira hiyo ilisisitizwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bw. Theobald Sabi, mbele ya Naibu Waziri wa Fedha, Bw. Laurent Luswetula (Mb), wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la maonesho ya benki hiyo katika Viwanja vya Usagara, mkoani Tanga, kunakofanyika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa. NBC ni miongoni mwa wadhamini muhimu wa maadhimisho hayo yaliyozinduliwa rasmi na Naibu Waziri huyo.

 

Akizungumza katika maonesho hayo, Bw. Sabi alisema NBC imeendelea kubuni na kuboresha huduma zake ili kukidhi mahitaji ya makundi mbalimbali, ikiwemo huduma za ndogo na kubwa, mikopo kwa wajasiriamali, mikopo ya kilimo, biashara na viwanda, pamoja na huduma za kifedha kwa taasisi na miradi mikubwa ya kimkakati ya maendeleo.

 

“Tunatambua kuwa ukuaji wa uchumi unahitaji mifumo imara ya kifedha. Ndiyo maana NBC tumejikita katika kutoa suluhisho rafiki za kifedha kupitia huduma za kidijitali, mikopo yenye masharti nafuu, pamoja na ushauri wa kitaalamu kwa wateja wetu ili waweze kukuza biashara na uzalishaji wao,” alisema Bw. Sabi.

 

Aliongeza kuwa benki hiyo imeendelea kuwekeza katika teknolojia za kisasa za kifedha (FinTech) ili kuongeza upatikanaji wa huduma hata kwa wananchi walioko maeneo ya vijijini, sambamba na kuimarisha ushirikiano na Serikali katika utekelezaji wa sera na mipango ya maendeleo ya Taifa.

 

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Fedha, Bw. Laurent Luswetula, aliwapongeza na kuzishukuru taasisi za kifedha ikiwemo benki ya NBC kwa mchango wao mkubwa katika kuimarisha sekta ya fedha nchini na kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza uchumi jumuishi.

 

“Serikali inaendelea kuhimiza taasisi za kifedha, kuja na bidhaa na huduma zitakazowagusa wananchi moja kwa moja. Tunashukuru kuona taasisi hizi zimewekeza zaidi jitihada zao katika katika huduma za kidijitali, mikopo kwa sekta za uzalishaji na kushirikiana na wadau mbalimbali katika maendeleo ya uchumi,” alisema Bw. Luswetula.

 

Alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa taasisi za kifedha ili ziweze kuchangia ipasavyo katika kukuza uchumi, kuongeza ajira na kuboresha maisha ya wananchi, huku akihimiza wananchi kutumia fursa za huduma za kifedha zinazotolewa na benki mbalimbali ikiwemo NBC.

Kwa upande wake, Meneja wa NBC Mkoa wa Tanga Bw Moses Charles alisema benki hiyo imejipanga kikamilifu kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa huo kwa kuzingatia fursa za kiuchumi zilizopo ikiwemo kilimo, biashara, viwanda vidogo na vya kati, pamoja na uwekezaji katika sekta ya bandari na usafirishaji.

Alisema mkakati wa NBC mkoani Tanga umejikita katika kuwawezesha wakulima na wajasiriamali kupitia mikopo maalum, huduma za kidijitali zitakazorahisisha miamala, pamoja na kutoa elimu ya kifedha kwa wananchi ili kuongeza uelewa na matumizi sahihi ya huduma za benki.

“Tunaamini Tanga ina nafasi kubwa ya kukua kiuchumi. Kupitia huduma zetu za kifedha, tunalenga kuwa mshirika wa karibu wa wananchi, wafanyabiashara na wawekezaji wa mkoa huu katika kufanikisha miradi yao na kuongeza ajira,” alisema Meneja huyo.

Naibu Waziri wa Fedha, Bw. Laurent Luswetula (Mb) (Kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi wakati Naibu Waziri wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la maonesho ya benki hiyo katika Viwanja vya Usagara, mkoani Tanga, kunakofanyika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa. NBC ni miongoni mwa wadhamini muhimu wa maadhimisho hayo yaliyozinduliwa rasmi na Naibu Waziri huyo. Wanaoshuhudia ni pamoja Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki hiyo Bw Godwin Semunyu (wa pili kushoto) na Meneja wa NBC Mkoa wa Tanga Bw Moses Charles (katikati)

Meneja wa NBC Mkoa wa Tanga Bw Moses Charles (katikati) akifafanua kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa wadau mbalimbali nchini wakiwemo Serikali, wafanyabiashara, wawekezaji, wajasiriamali, wafanyakazi, wakulima pamoja na makundi mengine ya kijamii mbele ya Naibu Waziri wa Fedha, Bw. Laurent Luswetula (Mb) (Kulia) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la maonesho ya benki hiyo katika Viwanja vya Usagara, mkoani Tanga, kunakofanyika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa. NBC ni miongoni mwa wadhamini muhimu wa maadhimisho hayo yaliyozinduliwa rasmi na Naibu Waziri huyo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kushoto) na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki hiyo Bw Godwin Semunyu (wa pili kushoto).


Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC, Bw. Theobald Sabi (katikati) sambamba na timu ya maofisa wengine wa benki hiyo akizungumza na kukabidhi  kwa baadhi ya wateja wa benki hiyo jijini Tanga wakati wateja hao walipotembelea Makao Makuu na matawi ya benki hiyo jijini  Tanga.





Baadhi ya maofisa wa benki ya NBC pamoja na maofisa wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania  wakiwahudumia wadau mbalimbali waliotembelea banda la benki hiyo katika Viwanja vya Usagara, mkoani Tanga, kunakofanyika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa. NBC ni miongoni mwa wadhamini muhimu wa maadhimisho hayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC, Bw. Theobald Sabi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na  timu ya maofisa wengine wa benki hiyo pamoja na  maofisa wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania kwenye banda la benki hiyo katika Viwanja vya Usagara, mkoani Tanga, kunakofanyika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa. NBC ni miongoni mwa wadhamini muhimu wa maadhimisho hayo.

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki ya NBC Bw Godwin Semunyu (Katikati) akijipongeza sambamba na  timu ya maofisa wengine wa benki hiyo wakiwa kwenye banda la benki hiyo katika Viwanja vya Usagara, mkoani Tanga, kunakofanyika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa. NBC ni miongoni mwa wadhamini muhimu wa maadhimisho hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...