Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Biashara wa BoA Bank, Hamza Cherkaoui akimkabidhi cheti cha shukrani kwa wateja wa SME wa Bank of Africa Tanzania.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha SME wa Bank of Africa Tanzania, Beatrice Richard akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Biashara wa Bank of Africa Tanzania, Hamza Cherkaoui (katikati), akisalimiana na mmoja kati ya wateja waliohudhuria mafunzo ya elimu ya fedha kwa wajasiriamali yaliyoandaliwa na benki hiyo,Jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Biashara wa Bank of Africa Tanzania, Hamza Cherkaoui, akifungua warsha ya Elimu ya Fedha kwa wajasiriamali (SME Clinic) yenye kaulimbiu “Kuwezesha Ukuaji Pamoja,”iliyofanyika jijini Dar es salaam juzi.
Viongozi na wafanyakazi wa Bank of Africa Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja na wateja wa SME baada ya mafunzo ya elimu ya fedha kwa wajasiriamali (SME Clinic) iliyolenga kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati, Dar es Salaam.


BANK of Africa Tanzania imeandaa warsha kwa ajili ya wajasiriamali iitwayo SME Clinic ambayo inalenga kutoa elimu ya masuala ya fedha ili kusaidia ukuaji wa biashara zao nchini kote.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Biashara wa Bank of Africa Tanzania, Hamza Cherkaoui, alisisitiza umuhimu wa Wajasiriamali katika kukuza uchumi wa Tanzania hasa kwenye masuala ya ajira na kuboresha maisha ya mtu mmoja mmoja. Akieleza dhamira ya benki alisema “Tumejikita kuhakikisha tunawawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati kwa kuwapatia maarifa, nyenzo na masuluhisho ya kifedha wanayohitaji ili kuendelea kustawi.”

“Bank of Africa Tanzania tumejikita kuhakikisha tunawapatia wajasiriamali wadogo na wa kati maarifa, nyenzo na masuluhisho ya kifedha wanayohitaji ili kustawi. Kupitia programu kama SME Clinic, tunajenga ushirikiano endelevu na wa kudumu na wateja wetu. Kwa kaulimbiu ya mwaka huu ‘Kuwezesha Ukuaji Pamoja’, tunadhihirisha dira yetu ya kuwa mshirika wa kifedha anayeaminika anayekua sambamba na wateja wake na sekta ya biashara za Tanzania,” alisema.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha SME wa Bank of Africa Tanzania akiongea katika warsha hiyo, alibainisha dhamira ya Benki katika kuwawezesha wajasiriamali kwa kuwapatia maarifa sahihi na suluhisho za kisasa za kifedha. Alieleza kuwa kupitia SME Clinic, benki inalenga kuwajengea uwezo wajasiriamali katika usimamizi bora wa fedha huku ikihamasisha matumizi ya mifumo ya kidijitali ili kurahisisha uendeshaji wa biashara zao.

Beatrice alisema benki inaendelea kutoa huduma rafiki za benki mtandao, ikiwemo BOAWeb/Internet Banking na B-Mobile, sambamba na kutumia mtandao wake mpana wa mawakala kuwafikia wateja popote walipo. Akigusia kaulimbiu ya “Kuwezesha Ukuaji Pamoja,” alisisitiza kuwa Bank of Africa Tanzania si mtoa huduma wa kifedha pekee, bali ni mshirika wa karibu wa wajasiriamali katika safari yao ya ukuaji endelevu na mchango wao katika maendeleo ya uchumi wa taifa.

Kaulimbiu ya mwaka huu, “Kuwezesha Ukuaji Pamoja”, inadhihirisha dhamira ya kwenda sambamba na wajasiriamali kuhakikisha si tu wanabaki sokoni, bali wanakua kwa njia endelevu na kuchangia kikamilifu maendeleo ya taifa. SME Clinic ya jijini Dar es salaam imewaleta pamoja wajasiriamali, wataalamu wa Bank of Africa Tanzania na wadau wa sekta mbalimbali kwa siku ya mafunzo, kubadilishana mawazo na kukuza ushirikiano.

Warsha hiyo hufanyika kila mwaka na inasisitiza dhamira yake ya utoaji wa elimu ya masuala ya kifedha inayolenga kuwawezesha wajasiriamali na kusaidia ukuaji wa biashara zao nchini kote.

SME Clinic ni sehemu ya Programu ya Elimu ya Fedha ya Bank of Africa Tanzania iliyoanzishwa mwaka 2021 kufuatia Kanuni za Ulinzi wa Watumiaji wa Huduma za Fedha za mwaka 2019. Kifungu cha 19 cha kanuni hizo kinahitaji kila mtoa huduma za kifedha kuandaa programu za elimu ya fedha kwa wateja wake.

Tangu ilipoanzishwa programu hii, imefanikiwa kuendesha warsha hizi (SME Clinics) katika mikoa ya Dar es Salaam,Dodoma, Mwanza na wilayani Kahama na tayari imeweza kuwafikia zaidi ya wateja 800.

Warsha hii pia inalenga kuboresha ujuzi katika usimamizi wa biashara kwa wateja, kuimarisha uhusiano kati ya Bank of Africa Tanzania na wateja wake, na kuhimiza matumizi ya mifumo na teknolojia za kidijitali ili kuongeza ufanisi wa biashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...