NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
CHUO Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), kupitia Shule Kuu ya Madini na Jiosayansi, kimepokea msaada wa kompyuta 10 kutoka Kampuni ya AngloGold Ashanti kwa ajili ya kuimarisha shughuli za ufundishaji na utafiti, ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 26, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya makabidhiano, Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa William Anangisye, amesema vifaa hivyo vitasaidia kuongeza ufanisi katika mchakato wa kujifunza, kufundishia na kufanya tafiti kwa wanataaluma na wanafunzi.
Amesema kupitia msaada huo, chuo kinatarajia kuendelea kuboresha mazingira ya elimu ya juu na kuchangia maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Aidha, Prof. Anangisye amezitaka taasisi na kampuni nyingine zinazojihusisha na sekta ya madini kujitokeza kutoa mchango wao kwa chuo hicho ili kusaidia kukijengea uwezo zaidi wa kutekeleza majukumu yake.
“Msaada wowote utakaotolewa utakuwa na mchango mkubwa katika kukisaidia chuo kufikia malengo yake ya kulielimisha taifa kwa manufaa ya maendeleo ya nchi,” amesema Prof. Anangisye.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Kampuni ya AngloGold Ashanti Kanda ya Afrika, Bw. Simon Shayo, amesema kukabidhi kompyuta hizo ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo kuhakikisha UDSM inakuwa na teknolojia inayokwenda sambamba na mahitaji ya sasa ya elimu na sekta ya madini.
Amesema uwepo wa kompyuta za kisasa chuoni hapo utasaidia kuwaandaa wanafunzi vizuri zaidi, ambao baadaye ni rasilimali muhimu kwa sekta ya madini na maendeleo ya nchi.
“Tunajenga wigo mpana wa ushirikiano kati yetu na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika maeneo ya ufundishaji, utafiti na ushauri wa kitaalamu,” amesema Bw. Shayo.
Ameongeza kuwa AngloGold Ashanti itaendelea kushirikiana na UDSM, ikiamini kuwa sekta binafsi ina jukumu la msingi katika kusaidia maandalizi ya wahitimu ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira na maendeleo ya taifa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...