Farida Mangube Mvomero, Morogoro
Vijana na wanawake wa vijiji vitano vikiwemo vya Lubungo, Mafuru na Mingo Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, wamepata fursa ya kujikomboa kiuchumi kupitia mradi wa uzalishaji wa mzao ya bustani kibiashara unaotekelezwa na Washirika wa Wahitimu Wajasiriamali wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUGECO).
Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano wa SUGECO na Programu ya Beyond Farming Collective (BFC), inayofadhiliwa na Bill na Melinda Gates Foundation.
Simtanu Yohane ni Afisa Kilimo huduma za Ugavi Wilaya ya Mvomero, amesema mradi huu utaleta mageuzi makubwa kwa jamii hasa kwa vijana na wanawake kwa kuwapata nafasi ya kujiajiri kupitia kilimo cha bustani kibiashara.
"Kilimo cha kisasa kitaongeza uzalishaji na kutoa masoko ya uhakika kwa mazao," alisema Afisa Kilimo huyo
Kwa upande wake Mkurugenzi wa SUGECO Bw. Revocatis Kimario amesema mradi huo umegharimu zaidi ya shilingi Bilioni . 13 fedha hizo zitatumika kuwekeza kwenye kilimo kupitia Kizimba Business Model katika kuweka miundombinu ya umwagiliaji, Teknolojia mpya na vifaa vya kisasa katika shughuli za kilimo ikiwemo matumizi ya nishati ya jua na mfumo wa umwagiliaji.
Kimario amesema mradi huo utakuwa na miundombinu yote ya uzalishaji wa kisasa hivyo ni wajibu wa vijana waliopata fursa kutumia mradi huo kuzalisha mazao ya bustan huku akiwahakikishia kuwepo kwa masoko ya uhakika wa mazao yatakayozalishwa.
"Kupitia Mradi huu ambao tumeweka miundombinu masingi ya kuwezesha uzalishaji tunampa kijana eneo la kuzalishia lenye miundombinu ya masingi, tumechimba visima 4 na mabwawa, kijana anapewa ekali moja hadi tatu na tunampa haki ya tumia eneo hilo kwa kipindi Cha miaka mitatu lengo letu ndani ya hicho kipindi Cha miaka mitatu azalishe auze na atengeneze Fedha anunue Ardhi yake na ajimilikishe yeye mwenyewe". Amesema Mkurugenzi wa SUGECO.
Nao wakazi wa Kijiji Cha Lubungo unaotekelezwa Mradi huo wamesema kupitia Mradi huo vijana watanufaika na mageuzi ya kilimo kwani awali walikuwa wanalima kilimo Cha msimu kwa kutegemea mvua.
"Sisi tunalima Mbaazi, nyama na mahindi lakini kilimo chetu ni chakutegemea mpaka msimu lakini ujio wa SUGECO na mradi wa kilimo Cha bustani sisi vijana Sasa tutanufaika nacho". Amesema Maneno Issa mkazi wa Lubungo
Mradi huo umedhaminiwa na Program ya Beyond Farming Collective (BFC) kwa ufadhili wa Bills and Melinda Gates Foundation umelenga kupanua mfumo wa kizimba Bussiness world Model (KBM) ambao unatekelezwa na Washirika wa Wahitimu wajasiliamali wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA (SUGECO).

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...