Watumishi wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida ambao ni Afisa Utumishi na Mhandisi wa Halmashauri hiyo wameelekezwa kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi na ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Mhe. Reuben Kwagilwa (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe (Mb), wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya elimu na barabara wilayani humo.
“Lengo la Mheshimiwa Rais ni kuhakikisha tunapata majengo yenye ubora, watoto wetu wanasoma katika mazingira mazuri na Serikali inapata thamani ya fedha sasa tukijenga kwa kulipua hivi ndani ya miaka mitano tutarudi tena kujenga, hii haikubaliki,” amesema Mhe. Kwagilwa.
Mhe. Kwagilwa amesema Afisa Utumishi Eliah Noah Samata amekuwa kikwazo kwa utendaji wa watumishi wengine kutokana na kushindwa kutimiza majukumu ya msingi ya kusimamia rasilimali watu, hali inayochochea uzembe kazini na kuchelewesha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Kwa upande wa Mhandisi wa Halmashauri hiyo, Bw. Innocent Magadula, amebainika kusimamia vibaya mradi wa ujenzi wa shule mpya ya msingi katika eneo la Shule ya Sekondari Grace Mesaki. Ametuhumiwa kuruhusu matumizi ya vifaa visivyokidhi viwango, ikiwemo kutumia changarawe badala ya mawe maalum katika sakafu za madarasa, hatua inayohatarisha uimara wa majengo na usalama wa wanafunzi.
Imebainika pia kuwa baadhi ya vipimo vya ujenzi vilivyokuwa kwenye makisio ya gharama (BOQ) vilipunguzwa bila kufuata taratibu, jambo linalokiuka miongozo ya Serikali na kuonyesha uzembe mkubwa katika usimamizi wa miradi ya maendeleo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...