RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan apokea Tuzo tatu za Utalii za “WORLD TRAVEL AWARDS” ambazo Tanzania imeshinda, Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ambayo Tanzania imeshinda kuwa eneo bora la Utalii wa Safari Duniani (World’s Leading Safari Destination) kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji, Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar tarehe 05 Januari, 2026. Tuzo hiyo imetolewa na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) yenye Makao Makuu yake Jijini London, Uingereza.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kabla ya kukabidhiwa Tuzo tatu ambazo Tanzania imeshinda katika Utalii, Afrika na Duniani. Kikao hicho kilifanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Januari, 2026. Tuzo hizo zimetolewa na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) yenye Makao Makuu yake Jijini London, Uingereza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha Tuzo ambayo Hifadhi ya Serengeti imeshinda kuwa Hifadhi bora Duniani (World’s Leading National Park, Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar tarehe 05 Januari, 2026. Tuzo hiyo imetolewa na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) yenye Makao Makuu yake Jijini London, Uingereza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande mara baada ya kupokea Tuzo 3 za Utalii za “WORLD TRAVEL AWARDS” ambazo Tanzania imeshinda, Ikulu Ndogo Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Januari, 2026.
Muonekano wa Tuzo tatu za “WORLD TRAVEL AWARDS” ambazo Tanzania imeshinda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...