Na WAF, Dar es Salaam

Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, ameipa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) muda wa miaka mitatu kuhakikisha hakuna Mtanzania anayekwenda nje ya nchi kutibiwa saratani.

Mhe. Mchengerwa ametoa kaulihiyo leo Januari 5, 2026 wakati wa uzinduzi wa Bodi ya ORCI, uzimduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam


"Tanzania chini ya Serikali ya awamu ya Sita ya Mhe. Samia Suluhu Hassan imepiga hatua kubwa na sasa ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika zenye huduma za kisasa za matibabu ya saratani hivyo lazima tuende na kasi ya Mhe. Rais amesema Mhe. Mchengerwa.

Kabla ya uzinduzi huo Waziri Mchengerwa, alikagua miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa na taasisi hiyo ikiwepo ufungaji wa mashine tatu mpya za matibabu ya saratani aina ya LINAC na Cobalt, upatikanaji wa mashine za kisasa za uchunguzi na matibabu ikiwemo PET CT, pamoja na uanzishaji wa kinu cha kuzalisha dawa za nyuklia (Cyclotron) kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.


Aidha, Waziri amekagua ujenzi wa jengo jipya la huduma za kimataifa linalolenga kuboresha huduma kwa wagonjwa wa ndani na nje ya nchi huku akipongeza Menejimenti ya ORCI kwa utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa Desemba, 2025 ya kuhakikisha mashine tatu za uchunguzi wa PET zinafungwa na kuanza kutoa huduma.

Katika ziara hiyo, Waziri Mchengerwa amezungumza na wagonjwa waliokuwa wakipatiwa huduma, ambapo kwa niaba yao Bi. Justina Allen amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha huduma za tiba ya mionzi na kusema kwa sasa wagonjwa wasio na uwezo wanapata matibabu bure baada ya kufuata taratibu zilizowekwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Dkt. Diwani Msemo, amesema kukamilika kwa ufungaji wa mashine mpya kutapunguza muda wa kusubiri huduma kutoka wiki 20 hadi takriban ni wiki mbili na kuongeza kuwa idadi ya wagonjwa wanaopata huduma kwa siku itaongezeka kutoka 200 na kufikia hadi zaidi ya 400.

Hata hivyo, Waziri Mchengerwa amesisitiza kuwa mageuzi ya huduma za saratani hayaishii kwenye majengo au mashine pekee, bali yaanze kwenye usanifu bora wa utoaji huduma kwa mgonjwa na kuboresha uzoefu wake wote wa matibabu na kuitaka ORCI kuwa wabunifu, jasiri na kuvunja mazoea ya zamani ili kuwa kituo cha ubora barani Afrika.
Sambba na hivyo Mhe. Mchengerwa amesisitiz matumizi ya teknolojia za kisasa, mifumo ya kielektroniki ya taarifa za wagonjwa na usimamizi thabiti wa Bodi, sambamba na kuimarisha utafiti na ushirikiano wa kitaifa na kimataifa, ili kuifanya ORCI kuwa taasisi inayoongoza katika matibabu na utafiti wa saratani.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...