Meneja Mkuu Shirika la Masoko ya Kariakoo CPA. Ashraph Abdukarim amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Chuo Kikuu cha Agakhan, mazungumzo hayo yamejikita kwenye uwekezaji wa miundombinu na uaznzishaji wa kituo cha kulea watoto katika Soko Kuu la Kariakoo.

CPA. Abdulkarim amewaeleza viongozi hao kuwa shirika limeandaa eneo zuri na kubwa ambalo endapo mwekezaji akijitokeza anaweza kujenga kituo hicho ambacho ujenzi wake ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa Februari 8, 2026 alifungua soko hilo rasmi.

CPA. Abdulkarim amebainisha kuwa kinachoendelea kwa sasa ni maandalizi ya michoro na taarifa ya kina kuhusu namna gani kituo hicho kiwe ambapo taarifa hizo zinaandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI baada ya kutembelea eneo hilo wakiwa na wataalam mbalimbali ambao waliambatana na wataalam wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Jiji la Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mkuu wa ujumbe huo kutoka Chuo Kikuu cha Agakhan, Prof Paschal Ruggajo ameushukuru uongozi wa Shirika la Masoko la Kariakoo kwa kukubali kukutana nao, kwani wanayo nia ya dhati ya kuanzisha kituo hicho kwa kutambua umuhimu wa afya na mazingira salama kwa mama na mtoto.

Naye, Dkt. Mariam Nooran ambaye ni Mkuu wa Idara ya Watoto Chuo Kikuu cha Agakhan ameonesha umuhimu wa kuwa na eneo la kunyonyesha na pia kulea watoto kwa pamoja na kubainisha kuwa yapo mambo mbalimbali yanapaswa kuzingatiwa ikiwemo usafi, usalama na mazingira yanayowapa fursa watoto kucheza.

Ikumbukwe kuwa Shirika la Masoko Kariakoo lilitenga eneo maalum kwa ajili ya wakina mama wanaofanya biashara katika Soko Kuu la Kariakoo kunyonyesha watoto wao, jambo ambalo limepata mwitikio mkubwa kutoka kwa jamii.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...