Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, amefungua rasmi Kikao kazi cha sita cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) leo 17 februari 2026 jijini Arusha huku akitilia mkazo ulinzi na usalama wa taarifa binafsi.

Akizungumza katika kikao hicho Dkt. Kusiluka amezitaka taasisi zote kuzingatia sheria na kujisajili kwenye taasisi ya ulinzi wa taarifa binafsi ili kuhakikisha zinahifadhiwa kwa usalama, pamoja na kuwasilisha taarifa ya miradi yote ya TEHAMA Serikalini, ambayo haikuzingatia Sheria, Kanuni na Viwango vya Serikali Mtandao ili hatua zichukuliwe kwa wahusika

Dkt. Kusiluka amesema Kila Mkuu wa taasisi ya umma, anawajibika kuhakikisha miradi yote ya TEHAMA katika taasisi yake inazingatia sheria mwaka 2019, Kanuni zake, Viwango na Miongozo yote ya Serikali kuanzia uanzishaji, usimamizi na uendeshaji wake,pamoja na kufuata taratibu zinazopaswa kufuatwa, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha andiko la mradi e-GA, kabla ya kuanzisha miradi hiyo.

Nawaelekeza kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa, wale wote watakaokaidi sheria hili watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria. Alisema

Aidha amesema Mafanikio ya Tanzania kutambuliwa kimataifa kupitia tuzo za Umoja wa Mataifa (UN Public Service Award), World Summit on the Information Society (WSIS), na tathmini ya Benki ya Dunia ya GovTech Maturity Index, ni ushahidi kuwa nchi ya Tanzania ipo katika

mwelekeo sahihi wa mageuzi ya Kidijitali Serikalini.Mafanikio haya si ya e-GA pekee,bali ni ya Serikali yote na Watanzania kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Serikali Mtandao (eGa) Benedict Ndomba katika hicho kilichudhuriwa na wajumbe 1400,wageni kutoka India Afrika ya Kusini ambacho kimebeba kaulimbiu isemayo kuboresha utendaji wa Serikali kwa kuimarisha utoaji wa huduma za umma kupitia mifumo salama na jumuishi ya Mtandao

Ndomba amesema kuwa Malengo ya kikao kazi hicho ni Kupanua wigo wa upatikanaji wa taarifa muhimu katika kila ngazi Serikalini, Kuimarisha usalama wa Serikali na raia wake katika karne ya sayansi na teknolojia na kuongeza uwezo wa Serikali kupambana na majanga kwa kutumia teknolojia ili kurahisisha michakato ya utendaji kazi kuanzia kwenye Wizara

Akitoa salam za mkoa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt.Toba Alnason Nguvila amesema kuwa, mkoa wa Arusha ni wadau wa matumizi ya Serikali huku Taasisi zote za binafsi na Serikali mkoani huo, zikitumia mifumo ya kidijitali katika kutoa huduma kwa wananchi, lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali na dhamira ya Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya matumizi ya kidijitali katika kutoaji wa huduma kwa wananchi.

Dkt. Nguvila amebainisha kuwa, Mamlaka ya Serikali Mtandao - eGA, ni wadau wa kuhamasisha matumizi ya mifumo ya kidijitali kwa Taasisi za Serikali nchini ambapo Mkoa wa Arusha ni wadau wakubwa wa Serikali Mtandao, kutokana na kuwa Taasisi zote za Serikali mkoani humo, ni watumiaji wazuri wa mifumo ya kidigitali kwa kuzingati ndio sera na maelekezo ya Serikali.

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ni taasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Serikali Mtandao namba 10 ya mwaka 2019 inayofanya kazi ya kuimarisha na kuendeleza utoaji wa huduma za serikali mtandao kwa taasisi za Umma ,lengo ni kuziwezesha Taasisi hizo kutumia TEHAMA katika majukumu yao ili kuongeza ufanisi, uwajibikaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...