Balozi Wilson Masilingi amesema kuwa masuala ya Uwazi na Uwajibikaji ni muhimu sana kwa manufaa ya wananchi,kwa kizazi cha sasa na hata kizazi kijacho.
Balozi Masilingi ameyasema hayo Jijini Dodoma Februari 17,2026 mara baada ya kupokewa katika Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini,Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) ambapo amepokewa kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Na kuongeza kuwa moja ya majukumu ya Taasisi hiyo ni pamoja na kuelimisha na kuwataarifu wananchi kuhusu mambo wanayoyafanya na matokeo yake na manufaa yaliyopo kwao.
"Kwasababu moja ya majukumu yetu ni kuwataarifu na kuelimisha wananchi waliotupatia jukumu hili kuhusu mambo ambayo tunafanya na matokeo yake na yana manufaa gani kwao na wanaweza kuchangia nini kuyaboresha kwa manufaa yao kwa kizazi cha sasa na kijacho,kama mnavyofahamu masuala ya Uwazi na Uwajibikaji ni muhimu sana sana".
Aidha ameahidi katika Uongozi wake kupitia Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo kuanza na Vijana walioko mtaani wenye taaluma kwenye masuala ya Madini,Mafuta na Gesi asilia kujisajili katika Website yao na wao kuona namna ya kuweza kuwafikia na kutafuta namna ya kuwafundisha zaidi ili waweze kusaidia kupata taarifa na kuhamasisha Umma ili kuondokana na jamii isiyoelewa mambo hayo.
Pamoja na hayo amesema anaamini Watumishi wa Taasisi hiyo watampatia ushirikiano kama walivyowapa watangulizi wake katika kutekeleza majukumu ambayo wamepewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya wananchi wake.
Pia Balozi Masilingi amewataka Watumisha hao kufanya kazi kwa bidii,umoja, kushirikiana na upendo kwani kwa kufanya hivyo kutaepusha kuwepo kwa migongano.
Mhe Balozi Wilson Masilingi ni Mwenyekiti wa 3 tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo ya TEITI.



.jpeg)

.jpeg)


.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...