Benki ya Exim Tanzania imeandaa hafla ya futari kwa wateja wake jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza na kuimarisha mahusiano yanayojengwa juu ya misingi ya uaminifu, uwajibikaji na maadili ya pamoja.

Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki, Bw. Jaffari Matundu, alisema kuwa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni wakati wa kutafakari na kukumbushana kuwa mafanikio ya kweli hujengwa juu ya maadili thabiti kama vile uaminifu, huruma na uwazi katika utendaji.

Benki ya Exim inathamini mahusiano na wateja wake zaidi ya miamala ya kifedha.

 “Dhamira yetu si kutoa huduma za kifedha pekee, bali kujenga imani, kupanua fursa na kugusa maisha ya watu kwa namna chanya,” alisisitiza.

Katika kuendeleza dhamira ya kuongeza ujumuishi wa kifedha nchini, Benki imeendelea kupanua mtandao wake kwa kufungua matawi katika maeneo ya Kahama, Ubungo na hivi karibuni Paje, huku mipango ikiendelea kuelekea Geita.

 Hatua hiyo inalenga kusogeza huduma karibu zaidi kwa wafanyabiashara, wajasiriamali na wananchi kwa ujumla.

Aidha, Benki ilithibitisha kuwa itaendelea kuwa mshirika wa kuaminika kwa wateja wake katika safari yao ya ukuaji na maendeleo ya muda mrefu.

“Uaminifu wenu kwetu ndiyo mtaji wetu mkubwa. Kila mara mnapochagua kufanya nasi kazi, mnatuwekea dhamana.

Na dhamana hiyo tunaichukulia kwa uzito na heshima kubwa.” Alisema Bw. Matundu.

Hafla hiyo iliwakutanisha viongozi wa dini, wateja pamoja na wageni waalikwa katika mazingira ya mshikamano, tafakari na kuimarisha ushirikiano kwa maendeleo ya pamoja. @exim_banktz 




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...