Na Hassan Kimweri, WAF - Dodoma
Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amewataka wanataaluma wa lishe nchini kutoa elimu sahihi kwa wananchi kwa viwango vinavyokubalika kupitia kwa makundi mbalimbali ikiwemo wana-habari, mama lishe, baba lishe ili jamii ione faida ya uwepo wa wanataaluma hao.
Dkt. Magembe amesema hayo leo Februari 26, 2026 alipokua anafungua Mkutano Mkuu wa Nne wa Chama cha Wataalamu wa Lishe Tanzania 2026 uliofanyika katika ukumbi wa Mabeyo Mkoani Dodoma.
"Sasa hivi, huko kwenye mitandao ya kijamii kuna watu wengi ambao hata hawajui chochote kuhusu lishe, lakini wako bize kila siku kutoa elimu ya lishe kwenye mitandao ya kijamii, mtaani, tusiwaache wale waongee kwa sababu wakati mwengine wanapotosha," amesema Dkt. Magembe
Amesema, jamii inatakiwa kupata elimu sahihi, ujumbe sahihi, kujua nini na kwa wakati gani chakula kipi kinafaa kuliwa, vitu gani visiliwe na kwa wakati gani, hii itapelekea kupata taifa lenye afya bora.
Aidha, Dkt. Magembe amewataka wanataaluma hao kufanya tafiti ili kujua tatizo la lishe nchini katika baadhi ya Mikoa na kujua kwa nini matatizo ya lishe yanayofautiana kati ya mkoa mmoja na mwengine.
"Hakuna taaluma yoyote katika Sekta ya Afya ambayo inaweza kwenda bila tafiti, tunakazi ya kufanya ili tujue tatizo ni nini, kwa nini mikoa yenye uzalishaji wa chakula ndio kuna udumavu," amesema Dkt. Magembe
katika hatua nyingine Dkt. Magembe ametumia fursa hiyo kuiasa jamii juu ya kupanda miti ya matunda pamoja na bustani za mbogamboga majumbani na hata katika vituo vya afya nchini










Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...