BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) linategemea katika robo ya tatu ya mwaka huu wa fedha kutembelea kamati za Michezo za Mikoa 12 ili kuthathimini utendaji kazi wa kamati hizo na kuhakikisha kamati hizo zimeundwa na zinatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kanuni za taasisi hiyo
Kamati za Michezo za Mikoa hujumuisha Afisa Tawala wa Mkoa husika, Afisa Michezo Mkoa, Wajumbe saba walioteuliwa na Mkuu wa Mkoa husika, mjumbe mmoja kutoka kila chama au shirikisho kilichosajiliwa katika mkoa huo pamoja na Maafisa Tawala wa Wilaya na Maafisa Michezo wote walioko katika Wilaya za mkoa husika.
Mkuu wa Kitengo cha Uendelezaji Michezo wa BMT, Benson Chacha amesema Kamati hizo za Michezo za Mikoa ndizo zenye jukumu la kutekeleza majukumu ya Baraza la Michezo la Taifa katika ngazi hizo ikiwamo usajili, kusimamia, kuendeleza vipaji, miundombinu, kuratibu mashindano n.k
Chacha amesema kamati zitakazotembelewa ni za Mikoa ya Kagera, Shinyanga, Simiyu, Mara, Mwanza, Geita, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Singida pamoja na Tabora.
Pia, amesema kuwa tathimini hiyo inalenga kuona utayari wa Kamati hizo jinsi zilivyo jipanga kuendeleza sekta ya michezo katika maeneo yao ili kongeza ajira, kuimarisha amani na mshikamano, kumasisha jamii kushiriki michezo, kuleta watu pamoja na kufikia matarajio ya Dira ya Taifa ya 2050.
Amesema, tathimini hiyo itaangalia namna ambavyo Kamati hizo zimechukua hatua madhubuti za kuimarisha utawala bora, uwazi na uwajibikaji katika kusimamia shughuli za Vyama na Mashirikisho ya Michezo kwenye mikoa husika ili viweze kuendeshwa kwa kuzingatia misingi ya kitaifa ya uendeshaji wa michezo hiyo nchini.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...