Tuzo hiyo imetolewa tarehe 13 Februari 2026, katika hoteli ya King Jada Dar es Salaam na taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na kutoa mafunzo, vyeti, na viwango vya taaluma ya huduma kwa wateja (customer service) na vituo vya kupokea simu (call centers inayoitwa Chartered Institute of Customer Management (CICM) Tanzania. 

Tuzo hii inaonesha namna MSD ilivyoboresha huduma zake kwa wateja kwa hasa za upatikanaji wa bidhaa za afya kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini. 

MSD hadi sasa inahudumia vituo vya kutolea huduma za afya 8,893 nchi nzima, huku vituo vyote vikipelekewa bidhaa hizo hadi mlangoni mara sita kwa mwaka.

Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji Hassan Ali ameeleza kuwa tangu kufanyika kwa maboresho Bohari ya Dawa, bidhaa za aina mbalimbali zimekuwa zikisambazwa kuendana na kasi ya uhitaji wa huduma hizo, ikiwemo mashine za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo,  mashine za usingizi na hata zile za kuwezesha huduma za afya ya kinywa na meno ambazo huduma zote hutekelezwa kwa kuzingatia misingi ya huduma kwa wateja iliyowekwa.

Ameongeza kuwa MSD ina mifumo ya kisasa ya kuwasiliana na wateja kama  vile Customer Portal, ujumbe wa simu (bulky sms), pamoja na Call Center ambapo zote hizi huwezesha kuwasiliana na wateja na kutatua changamoto mbalimbali.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...