TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imeendelea na vikao vyake leo Februari 14, 2026 kwa kukutana na Balozi wa Kudumu wa Tanzania Ofisi rasmi za Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswiswi, Dkt Abdallah Possi na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Ufalme wa Ubelgiji na Mkuu wa Ubalozi wa Tanzania kwa Umoja wa Ulaya (EU), Jestas Nyamanga.

Mkutano huo wa Tume na Mabalozi hao umefanyika katika ukumbi wa Tanganyika uliopo jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani hapa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Tume kukusanya taarifa, maoni na ushauri kutoka kwa viongozi mbalimbali.

Kwa Pamoja Balozi Possi na Balozi Nyamanga walijadili namna matukio ya uvunjifu wa amani yalivyoanza, athari zake kwa wananchi, mali zao na miundombinu, pamoja na mapendekezo ya namna ya kudhibiti na kuzuia matukio kama hayo yasijirudie siku zijazo.

Vilevile, katika mkutano huo hoja zilizojadiliwa zilihusu maeneo ya tathmini ya athari za matukio hayo na ushauri wa hatua za kijamii na kisheria zinazoweza kuchukuliwa ili kuimarisha amani na mshikamano wa kitaifa.

Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali ikiwemo waathirika wa matukio ya uvunjifu wa amani katika mikoa tofauti nchini, kwa lengo la kukusanya ushahidi na taarifa zitakazoiwezesha kuandaa ripoti ya kina.







 

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...