MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo ameamsha shangwe baada ya kufanikiwa kumaliza mgogoro wa ardhi wa muda mrefu ulihusu eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya maakaburi kuvamiwa na kujengwa nyumba za makazi ya watu.
Eneo lilovamiwa lipo Kimani Mtaa wa Kinyamwezi, Kata ya Pugu, Ilala Jijini Dar es Salaam ambapo wakazi wa eneo hilo walimtuhumu Elizabeth Mwakapangala kuliuza huku akifukua makaburi bila ya kufuata sheria.
Mpogolo akizungumza na wananchi wa eneo hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Februari 13, 2026 ambao ulihudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuhuruma Mabelya alisema eneo hilo lilitengwa na Serikaali kwa ajili ya makaburi.
“Eneo hili lenye ramani ya upimaji namba E' 351\96, ya mwaka 2000, Kiwanja Na. 423 Kitalu N Pugu Mwakanga Kata ya Pugu Halmashauriya Jiji la Dar es Salaam lilitengwa kwa matumizi ya makaburi kwa mujibu wa mipango miji, lakini baadhi ya yetu yaani Mama Elizabeth alifungua kesi ya ardhi namba 202/2020 kati yake Elizabeth Mwakapangala ambaye alikuwa msimamizi wa mirathi ya Saidi Shomari Loko akiipeleka Halmashauri ya Jiji, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mahakamani,” alisema Mpogolo.
Mpogolo akisoma hukumu katika mkutano huo iliyotolewa na Mhe. Jaji A. M. Msafiri aliyesikiliza kesi hiyo ilielekeza mlalamikaji Bi Elizabeth alipwe fidia na siyo kuuza eneo la makaburi wala kufukua makaburi ya watu na kutupa mabaki ya miili hiyo dampo kama alivyofanya.
Aidha, Mhe. Jaji Msafiri alitoa muongozo mzuri kwa mlalamikaji wa namna ya kupata haki yake ya fidia na kueleza kuwa Mahakama haina mamlaka ya kufuta ramani ya mipango miji iliyoandaliwa na Serikali au kuhoji mamlaka ya Rais ya kutwaa ardhi kwa manufaa ya umma.
Mpogolo alisema kufuatia hukumu hiyo mlalamikaji hakuwa na haki ya kuuza eneo hilo wala kuhamisha makaburi na nikinyume na katazo la Sheria ya Mipango Miji katika Kifungu cha 3 (e) cha sheria hiyo.
Akisisitiza katika mkutano huo Mpogolo alisema uhamishaji wa makaburi upo kwa mujibu wa sheria za nchi na kueleza kuwa mtu yeyote hawezi akatoka na maamuzi ya kikao cha familia na kwenda kuhamisha mwili wa mtu aliyezikwa kwenye kaburi husika ni lazima afuate utaratibu uliopo kisheria na miiko ya dini zetu.
Alisema mlalamikaji Elizabeth anapaswa kufuata utaratibu wa kisheria ili pate haki yake na si vinginevyo.
Mpogolo alisema awali mlalamikaji alisimamishwa kufanya chochote kwenye eneo hilo analodai ni lake lakini hakufuata maelekezo na sasa Serikali imekata rufaa uamuzi wa Mahakama na kuhusu kufukua Makaburi na kutupa mabaki ya miili wanakwenda kushughulika naye kwa mujibu sharia.
Aidha Wananchi hao wamedai kuwa eneo lenye mgogoro lilitengwa kwa ajili ya maziko, kama walivyoelekezwa na serikali ya mtaa na watu waliohamishwa kutoka Kipawa kupisha upanuzi wa Uwanjani wa Ndege wa Mwalimu Nyerere.
Leo amefika akiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuhuruma Mabelya kwa lengo la kuwasikiliza wananchi hao na kuamuru kuwa wananchi hao wawe ma amani na waendelee na shughuli zao ambazo zimepangiwa na serikali kwa eneo hilo.
Akizungumza Mama Elizabeth, amekanusha madai hayo akieleza kuwa hajawahi kufukua makaburi hayo na kwamba eneo hilo siyo eneo la Makaburi na ni mali yake halali ambalo anazo nyaraka zote baada ya kushinda kesi mahakamani tarehe 20 Oktoba 2022.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...