-Akagua ujenzi wa Chuo cha VETA Same.

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Matokeo na amedhihirisha hayo katika kipindi chake cha uongozi.

Amesema hayo leo Februari 18, 2026 alipokagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Chuo cha VETA katika Wilaya ya Same, Tarafa ya Chome Suji Kata ya Makanya.

Ujenzi wa Chuo hicho utagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 1.4 kutoka Serikali kuu ili kukamilisha ujenzi wa Chuo hicho kwa awamu ya kwanza na mpaka sasa kiasi cha Shilingi milioni 542 kimeshapokelewa Wilayani hapo

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani kulikuwa na wilaya zaidi ya 60 ambazo hazikuwa na mradi wowote wa VETA lakini alielekeza wilaya zote ambazo hazina VETA zijengwe ikiwemo na mikoa isiyokuwa na vyuo hivyo”

“Lakini pia alikuta kuna Wilaya zaidi ya 119 hazina hospitali za Wilaya, pia alikuta zaidi ya kata 649 hazikuwa na vituo vya afya, ndani ya kipindi chake amejenga hospitali zote 119 za Wilaya pamoja na vituo 649 kwenye tarafa na kata za kimkakati”

Aidha, Dkt. Mwigulu amesema kuwa Rais Dkt. Samia amejenga zaidi ya shule za Sekondari 1300 ikiwemo shule maalum kwa Wasichana kwenye kila Mkoa “Pia amejenga shule za Msingi 2700 pamoja na kujenga madarasa 79,000 kwa ajili ya watoto wa Kitanzania”

Kuhusu ujenzi wa barabara ya Makanya - Chankonko - Mvungo yenye urefu wa km 33, amewaelekeza Halmashauri hiyo wafuate taratibu ili ihamishiwe Wakala wa Barabara (TANROADS) kwani ikibakia TARURA na kuendelea kujengwa kilomita moja au mbili haitamalizika. Barabara hiyo inapitisha magari makubwa yanayobeba mizigo ya jasi.

Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa ujenzi wa chuo hicho utasaidia kuzalisha rasilimali watu itakayochagiza kuleta maendeleo katika Sekta sekta mbalimbali ikiwemo Viwanda.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...