Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameipatia tuzo Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa kutambua mchango wake na unaotolewa na Mamlaka hiyo katika usimamizi wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini.

Tuzo hiyo iliyotolewa wakati wa Usiku wa Tuzo za Umahiri katika Sekta ya Maji, tarehe 23 Februari jijini Arusha, ilipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile.

Akizungumza baada ya kukabidhi tuzo hiyo, Mhe. Aweso alieleza kuwa, lengo ni kutambua utendaji bora wa mamlaka za maji, wasimamizi na watendaji katika maeneo waliofanya vizuri kwa kipindi cha miaka mitatu (2021/22, 2022/23 na 2023/24).

Akizungumza baada ya kupokea tuzo, Dkt. Andilile, alisema kuwa EWURA itaendelea kushirikiana na Wizara ya Maji pamoja na kuzisimamia kwa uthabiti ili ziendelee kufanya vizuri katika utoaji wa huduma.

  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...