Mkutano wa 6 wa Serikali Mtandao umemalizika Februari 19, 2026, huku Halmashauri ya Wilaya ya Geita ikitangazwa kuwa Mshindi Namba Moja kati ya Halmashauri 184 nchini katika matumizi bora ya mifumo ya kiserikali kwa kuzingatia sheria, viwango na miongozo inayotolewa na Mamlaka ya Serikali Mtandao.
Tuzo hiyo imetolewa katika Mkutano wa 6 wa Serikali Mtandao uliofanyika katika ukumbi wa Arusha International Conference Centre (AICC), jijini Arusha na kukabidhiwa na Mhe Ridhiwani Kikwete, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati akifungua Kikao hicho cha 6.
Mkutano huo wa siku 3, ulifunguliwa rasmi Februari 17, 2026 na Mhe Moses Mpogole Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) ambapo amesema Nchi ya Tanzania ipo katika muelekeo sahihi wa mageuzi ya kidijitali. "Mimi naiona Tanzania nzuri sana wala sio baadaye sana ni hivi Karibuni" Amesema Balozi Dkt Kusiluka.
Vile Vile Katibu Mkuu Kiongozi amesema Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye TEHAMA na hii ni kwa kutambua kuwa maendeleo ya sasa hayawezi kupatikana nje ya mifumo ya kidijitali.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Karia Magaro, ameishukuru Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGa) kwa kutambua juhudi hizo, na amekipongeza Kitengo cha TEHAMA kwa usimamizi madhubuti wa mifumo ya kiserikali inayowezesha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
"Tuendelee kujikita kwenye mifumo na kuongeza kasi katika mifumo yote inayoletwa na Serikali" Amesema Magaro.
Naye Mkuu wa Kitengo Cha TEHAMA, Halmashauri ya Wilaya ya Geita Frank Makonda ametoa rai kwa watumishi wa Halmashauri kuendelea kushirikiana na kuongeza bidii kwenye ubunifu wa kutoa huduma kwa wananchi kwa kufuata Sheria na miongozo inayotolewa na Mamlaka ya Serikali Mtandao.
Ushindi Huo wa Tuzo hiyo (Best Performance in Compliance to e-Government Act, Standards and Guidelines) ni ushahidi kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita chini ya Mkurugenzi Mtendaji Karia Rajab Magaro, inaongoza kwa ubunifu, uwazi na matumizi sahihi ya TEHAMA katika utumishi wa umma.
Kikao hicho kimeongozwa na Kauli Mbiu isemayo " Kuboresha utendaji wa Serikali kwa kuimarisha utoaji wa huduma za umma kupitia mifumo salama na Jumuishi ya Serikali Mtandao.

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...