Leo tarehe 20.2.2025 Mkuu wa mkoa wa Rukwa. Mhe. Makongoro Nyerere ametembelea Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na kuwasilisha pongezi zake kuwa Tangu kuanzishwa kwake TADB ni benk ambayo imekuwa kwa kasi kubwa ndani ya miaka kumi (10) ikihudumua wakulima, wafugajo na wavuvi ambao mkoani Rukwa wapo na wanategemea mikopo ya benki hii kwa masharti ya riba nafuu.

Akipokea ugeni huo Bw. Frank Nyabundege Amempongeza Mhe. RC kwa kuaminiwa na kuteuliwa na Mhe Rais kuwa mkuu wa mkoa wa Rukwa.

Aidha amemuelezea kuwa mafanikio ya Benk ya TADB yametokana na jitihada za Serikali awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuiongezea benk fedha katika mtaji wa benki ili kufikia wakulima, wafugaji na wavuvi wengi hapa nchini.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...