Kocha wa Kagera Sugar Juma Kaseja
Na Khadija Kalili, Kibaha
TIMU ya soka ya Kagera Sugar ya Bukoba jana wametoka kifua mbele kwa ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Timu ya Transint Camp kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza waliocheza mwishoni mwa wiki katika Uwanja wao wa Nyumbani Filbert Bayi Mkuza Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mechi hiyo kumalizika Kocha wa Kagera Sugar Juma Kaseja 'Tanzania One' amesema kuwa licha ya ushindi huo kuna maboresho yanahitajika hasa kwa waamuzi ili wachezeshe mpira kwa kuzingatia maadili na kanuni za mpira.
"Tunaposema tunahitaji maboresho ya viwanja siyo kwamba viwanja ni vibaya la hasha, tunahitaji marefarii watoe maamuzi ya sahihi ni hivyo tu," amesisitiza Kaseja.
"Mchezo ulikuwa mgumu hasa katika kipindi cha kwanza hadi tunakwenda mapumziko Transit Camp walikuwa wanaongoza kwa goli moja na kwamba timu zote zilikuwa zimekamiana kimchezo".
Kaseja amesema wamejipanga katika michezo yake ijayo watajipanga ili wapate matokeo mazuri zaidi.
Naye Kocha wa Timu ya Transit Camp Shadrack Nsajigwa amekiri kuzidiwa kete na Kagera Sugar pia amewapongeza wa kunyakua pointi tatu.
"Kagera Sugar wamefanya vizuri katika kipindi cha pili mimi na wachezaji wangu tutaanza mazoezi Jumatatu huko ndiko tutajua namna ya kutafuta mbinu za kushinda" amesema Nsajigwa.
Kwa upande wake Kapteni wa Timu ya Transit Camp Isa Dau amekiri kushindwa na kuwapongeza Kagera Sugar, kwa kusema walizidiwa katika kipindi cha pili ambapo wenzao walizitumia vizuri nafasi na kufanikiwa kuwafunga.
Kapten wa timu ya Transit Camp Isa Dau.


.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...