-Lengo ni kufikisha umeme kwenye vitongoji vyote nchini ifikapo 2030

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unaendelea kutekeleza miradi ya kusambaza umeme vitongojini kwa lengo la kuhakikisha ifikapo Mwaka 2030 vitongoji vyote viwe vimefikishiwa umeme.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa REA, Meneja wa Usimamizi wa Miradi ya Kusambaza Umeme REA, Mha. Deogratius Nagu ameyasema hayo Mkoani Ruvuma Februari 1, 2026 wakati wa ziara ya kukagua miradi ya kusambaza umeme inayotekelezwa mkoani ili kujionea hali ya utekelezaji.

“Tupo katika Mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali ya kusambaza umeme vitongojini inayotekelezwa na Wakala na leo hii tumefika hapa Wilayani Mbinga kukagua mradi wa kupeleka umeme vitongoji 148 ujulikanao kama Mradi wa Ujazilizi Fungu 2C (Densification 2C) unaohusisha Wilaya ya Songea, Mbinga na Nyasa,” amefafanua Mhandisi Nagu

Katika ziara hiyo, Mha. Nagu amemuelekeza Mkandarasi anayetekeleza mradi, kampuni ya MF Electrical Engineering Ltd kuhakikisha anaongeza kasi ya ujenzi wa mradi ili akamilishe usambazaji wa umeme katika vitongoji 60 vilivyosalia katika mradi huo.

“Huu mradi unahusisha usambazaji umeme katika vitongoji 148 ambapo vitongoji 88 tayari vimewashwa umeme na kubakiza vitongoji 60 ambavyo utekelezaji unaendelea; tumemuelekeza Mkandarasi kuhakikisha anakamilisha mapema kazi ya kusambaza umeme katika vitongoji alivyobakiza,” amesema Mha. Nagu.

Akizungumza kwa niaba ya Msimamizi wa Miradi ya REA Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Zakaria Ng’okorome amesema mradi unatekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 18.294 na kwamba utanufaisha wateja wa awali wapatao 6,781.

Naye Msimamizi wa Mradi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ruvuma, Mha. Ali Pandit alisema wamejipanga kikamilifu kuhalkikisha miradi inakamilika kwa wakati na kufikisha umeme kwa wananchi.

Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi upande wa Mkandarasi, Mha. Musa David amesema wamepokea maelekezo na kuahidi kukamilisha mradi kwa wakati.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...