Shirika la Masoko ya Kariakoo kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Ukoaji Mkoa wa Kizimamoto Ilala imetoa mafunzo ya zimamoto na uokoaji kwa watumishi wa Shirika hilo na wafanyabiashara zaidi ya 400 ambao wanafanya biashara katika Soko Kuu la Kariakoo.
Akifungua mafunzo hayo, Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo CPA. Ashraph Abdulkarim amesema kutolewa kwa mafunzo hayo ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa Februari 8,2026 wakati wa ufunguzi wa soko hilo la kimataifa.
“Ninawashukuru wafanyabiasha wa Soko la Kariakoo na wafanyakazi kwa kujitokeza kwa wingi katika mafunzo haya, Mhe. Rais aliona mifumo na miunombinu ya kisasa ya kuzima moto na kutaka wafanyabiashara kujengewa uwezo wa namna ya kutumia mifumo hiyo kwa usalama wa soko na wafanyabiashara wote hvyo tumetekeeza” CPA. Abdulkarim
Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Ilala, ACF. Chrispin Rabiuzima amesema wafanyabiashara na watumishi waliopatiwa mafunzo hayo wanatakiwa kuwa wakufunzi kwa wengine kwa kuwa mafunzo hayo yametolewa kwa sehemu ya wafanyabiashara Zaidi ya 1800 ambao wanatoa huduma sokoni hapo.
ACP. Rabiuzima amebainisha kuwa mafunzo hayo yamelenga kuondoa hofu na kuelewa vema namna ya kutumia miundombinu ya zimamoto ilipo sokoni na kuitumia kwa usahihi na kuwaongoza wafanyabiashara wenzao pale changamoto yoyote itakapojitokeza sokoni hapo

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...