Na FARIDA MANGUBE MOROGORO
Waziri wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Kitila Mkumbo, ameweka wazi kuwa kilimo kinabaki kuwa sekta muhimu ya uchumi wa taifa na kwamba ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ni lazima sekta hiyo ilindwe, itunzwe na kuendelezwe kwa ushirikiano wa dhati kati ya wananchi, serikali, na wawekezaji.
Waziri Mkumbo ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro ambapo amekagua maendeleo ya uwekezaji wa kilimo katika maeneo hayo.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkumbo alijikita zaidi katika kuimarisha ulinzi wa miundombinu ya kilimo, akisema kuwa serikali inatoa kipaumbele kwa kilimo cha kibiashara, ambacho kimejikita katika uzalishaji wa mazao ya mtama, mahindi, miwa, ufuta na alizeti.
Amesisitiza kuwa, licha ya kuwa na ardhi kubwa inayofaa kwa kilimo, bado Tanzania inakosa tija, huku sehemu kubwa ya ardhi hiyo ikiwa haijalimiwa.
“Tunahitaji ushirikiano wa kila mmoja. Bila usalama, kilimo cha kibiashara hakiwezi kustawi. Wawekezaji hawa wamewekeza fedha nyingi, lakini changamoto hizi zinapunguza tija na athari zake ni kubwa kwa uchumi wetu,” alisema Mkumbo.
Aliongeza kuwa, kwa upande wa serikali, miongozo ya kisera imejikita katika kuboresha mazingira ya biashara, lakini bila ushirikiano wa jamii na wawekezaji, juhudi hizo zitakuwa bure. Alisema kuwa, kilimo kimekuwa sekta ya kujikimu kwa muda mrefu, lakini sasa serikali inalenga kuhamasisha kilimo cha kibiashara, ili kuongeza uzalishaji wa mazao na kutoa ajira kwa wananchi wengi.
Madiwani wa kata za Matuli na Mkulazi wamekiri changamoto zinazozikumba sekta ya kilimo, lakini walisisitiza kuwa jamii ina nafasi kubwa katika kuhakikisha kuwa changamoto hizi zinatatuliwa.
Madiwani hao walieleza kuwa, ili kufanikisha mabadiliko ya kilimo cha kibiashara, ni lazima wananchi washirikiane kwa karibu na wawekezaji na mamlaka za serikali.
“Kilimo ni fursa kubwa kwa wananchi wetu. Lakini ili kufanikisha hili, tunahitaji kushirikiana na wawekezaji ili kuimarisha usalama wa maeneo ya uzalishaji na kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija,” alisema Lucas Lemono, Diwani wa Kata ya Matuli.
Katika kuimarisha kilimo cha kibiashara, Waziri Mkumbo amesema kuwa Serikali itaendelea kutekeleza mkakati wa kuvutia wawekezaji wa ndani na nje, kwa kutoa mikopo nafuu na mafunzo kwa wakulima wadogo, huku ikiwataka wawekezaji kutumia teknolojia za kisasa ili kuongeza uzalishaji na tija.
Amesisitiza kuwa ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, sekta ya kilimo inahitaji uwekezaji wa kutosha katika mashamba makubwa, matumizi ya teknolojia za kisasa, na mitaji ya kutosha.
“Kilimo cha kisasa kinahitaji vifaa vya kisasa, mbegu bora, na mifumo ya umwagiliaji.
Wawekezaji hawa wanatakiwa kusaidia wakulima wadogo kwa kuwapa mafunzo na mitaji, na serikali iko tayari kutoa msaada wote unaohitajika,” alisema Mkumbo.
Meneja Mkuu wa Santagro Ltd, Luab Luiz de Carvalho, ameiomba serikali Kumalizia changamoto ya muingiliano kati yao na wafugaji ambapo wafugaji wamekuwa wakiingiza Mifugo shambani na kulisha mazao. Alisema kuwa, licha ya kuwa na miundombinu imara, mifugo ni tishio kubwa kwa uwekezaji wao.
“Tunahitaji msaada wa haraka kutoka kwa serikali na jamii kuhakikisha mifugo inadhibitiwa. Bila ulinzi wa kutosha, hakuna uwekezaji wa maana utakaofaidi jamii,” alieleza de Carvalho.
Ziara hiyo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mussa Kilakala, ambaye alihakikishia wawekezaji kuwa, pamoja na changamoto, Wilaya ya Morogoro ni eneo salama la uwekezaji na kwamba usalama wa maeneo ya kilimo utadumishwa kwa nguvu zote.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...