Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda, ameweka wazi kuwa, Kocha Miguel Gamondi amesaini rasmi mkataba wa kuifundisha timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars).
Waziri Makonda amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, leo Februari 16, 2026, wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Kocha huyo iliyofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Amesema kuwa Gamondi amestahili mkataba huo baada ya kuonesha uwezo wa hali ya juu katika michuano ya AFCON 2025 iliyofanyika Morocco hivi karibuni na kuingoza Taifa Stars kufika hatua ya 16 ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania akiwa kocha wa muda.
Serikali sasa imeamua kumwajiri rasmi ili aiongoze timu hiyo katika jitihada za kunyakua ubingwa wa AFCON 2027, ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo.



.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...