Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera , Bunge ,Uratibu na Wenye Ulemavu  Ummy Nderiananga  amesema Tanzania inaungana na nychi nyingine duniani katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Breli na maadhimisho hayo hufanyika katika halmashauri zote nchini kwa ngazi ya Kitaifa .

Mh. Ummy ameogeza kuwa maadhimisho hayo yatafanyika Kitaifa  katika  Mkoa wa Tanga na kuhusisha shughuli mbalimbali ikiwemo Maonyesho ya teknolojia na kazi za wasioona, upimaji wa elimu na Ujenzi  wa wasioona, kongamano la wadau na jamii ya na shughuli za burudani na hotuba na viongozi wa Serikali na wadau. 

Mh. Ummmy amezungumza hayo kuelekea maadhimisho ya siku ya  Breli nchini yatakayofanyika  Mkoani Tanga tarehe 12 February 2026 akiwa na waandishi wa habari katika  ukumbi wa ofisi hizo jijini Dodoma leo,  akitoa tamko hilo huku  kauli mbiu ya Shughuli hiyo ni "Teknolojia ya breli husaidia kuchochea kwa wasioona na ujenzi wa Taifa."

Nderiananga ameongeza kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za wenye ulemavu hususani wasioona wanapata haki ,fursa na huduma sawa kama wananchi wengine ikiwemo kiuchumi,kijamii,kisiasa na kitamadu hi pia kuwapa sera ya Taifa  ya maendeleo ya huduma na mafunzo ya mwaka 2004 sera ya Elimu ya Taifa mafunzo ya 2014 toleo la  2023, sera ya ajira ya mwaka 2008 pamoja na utekelezaji wa sheria ya watu wenye ulemavu.

Kwa upende wake katibu wa chama cha wasioona Mkoa wa Dodoma Enock Mbawa amesema ushiriki wa watu wenye ulemavu unafanya watu wengine waamke kwa kusoma kwa bidii kufanya kazi kwa bidii  na kujitoa katika makongamano mbalimbali ambayo ya nahusisha watu wasioona na walemavu wengine mfano Naibu Waziri Nderiananga na kuelekeza pongezi nyingi kwa Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...