Samsung Electronics East Africa imezindua rasmi maduka mawili mapya ya chapa ya Samsung katika maeneo ya Kunduchi na Ubungo, hatua inayothibitisha uwepo thabiti wa Samsung nchini Tanzania na kuimarisha ahadi yake ya kuwaletea wateja uzoefu kamili wa teknolojia inaounganisha watu wote.

Maduka haya yamefunguliwa ili wateja waweze kuona bidhaa zote za Samsung chini ya paa moja, likiweka pamoja simu za mkononi na vifaa vya elektroniki katika eneo moja. 

Kupitia Maduka haya, yanawapa wateja nafasi ya kuona na kujaribu bidhaa zote za Samsung, kutoka simu, kompyuta, televisheni, hadi vifaa vya nyumbani na vya kuvaa, na kuona jinsi zinavyorahisisha maisha ya kila siku.

Sherehe za uzinduzi zilihudhuriwa na wadau muhimu wa sekta, washirika wa biashara, pamoja na wanahabari,ikionyesha umuhimu wa uwekezaji huu kwa soko la kidijitali na rejareja Tanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkuu wa Kitengo cha Simu za Mkononi wa Kampuni ya Samsung Electronics East Africa ( Tanzania) Mgope Kiwanga alisema:“Ufunguzi wa maduka haya mapya ya Kunduchi na Ubungo ni hatua muhimu katika kuwaletea wateja wetu uzoefu kamili wa Samsung.

 Hapa, wateja wanaweza kuona jinsi simu zetu na vifaa vya nyumbani vinavyoshirikiana kwa pamoja, na jinsi teknolojia inavyoweza kufanya maisha kuwa rahisi na yenye kuleta maana kila siku,” alisema Kiwanga.

Tofauti na maduka ya kawaida, maduka haya ni makubwa na yametengenezwa kwa lengo la kuleta utofouti wa bidhaa za Samsung. Hapa wateja wanaweza kuona bidhaa zote pamoja, kujaribu na kuelewa jinsi zinavyorahisisha mawasiliano, burudani na shughuli za nyumbani.

Maduka pia yanatoa elimu kwa vitendo ya namna ya kutumia Vifaa vya Samsung  , msaada wa kitaalamu kutoka kwa wafanyakazi waliofunzwa na Samsung, upatikanaji wa vifaa halisi na huduma bora baada ya mauzo, ili wateja sio tu wanunue bidhaa, bali pia kuelewa jinsi ya kutumia kikamilifu bidhaa za Samsung.

Meneja wa Kitengo Cha Biashara kutoka Samsung Tanzania Daesong Ra alsema uwekezaji huu ni endelevu unalenga kuchangia mageuzi ya kidijitali na ukuaji wa Uchumi nchini Tanzania: “Ufunguzi wa maduka haya mawili unaonyesha imani ya Samsung katika soko la Tanzania. 

Uwekezaji kama huu unapanua upatikanaji wa teknolojia, kuunda ajira na kuendeleza ujuzi wa wafanyakazi wa hapa, jambo ambalo ni muhimu kwa maendeleo ya taifa,” alisema Daesong Ra.

Mbali na kuboresha uzoefu wa wateja, maduka haya mapya pia yanachangia ukuaji wa uchumi wa ndani kupitia ajira na mafunzo kwa wafanyakazi wa Tanzania, ikiwajengea ujuzi wa hali ya juu kama Samsung-certified, kuhakikisha huduma bora na kuendeleza vipaji vya ndani.

Maduka haya mapya yanathibitisha ahadi ya Samsung kwa wateja wake Tanzania, huku wateja wakiwa na nafasi ya kupata uzoefu wa bidhaa zote na teknolojia mpya kwa urahisi.




 

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...