Shirika la MyLEGACY limekutana na waandishi wa habari na wadau wa vyombo vya habari katika kikao cha ushirikishwaji chenye lengo la kuimarisha uelewa wa umma kuhusu mabadiliko ya tabianchi na kuiweka sekta ya habari kama jukwaa muhimu la utetezi wa masuala ya mazingira na usawa wa kijinsia.
Kikao hicho ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Kukuza Hatua za Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi Zinazozingatia Usawa wa Kijinsia kwa Kesho iliyo Bora (Kesho Njema) unaotekelezwa kwa msaada wa Embassy of Ireland in Tanzania.
Akizungumza katika kikao hicho, mwakilishi wa MyLEGACY amesema jamii nchini zinaendelea kukabiliwa na athari za mabadiliko ya tabianchi zikiwemo mafuriko, ongezeko la joto la muda mrefu na uhaba wa maji, hali inayoathiri zaidi wanawake, wasichana na watu wenye ulemavu.
Imeelezwa kuwa mabadiliko ya tabianchi yanaongeza pengo la kijinsia, yanaongeza hatari za ukatili wa kijinsia na kuvuruga upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi.
Hata hivyo, mifumo mingi ya mipango ya kukabiliana na tabianchi bado haijaingiza kikamilifu mwelekeo wa kijinsia katika tathmini ya udhaifu na ustahimilivu wa jamii.
Tathmini Yabaini Mapungufu katika Mipango ya Tabianchi
Kupitia mradi wa Kesho Njema, MyLEGACY imefanya tathmini ya mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, kwa kuangazia jinsi inavyojumuisha haki za afya ya uzazi na hatua za kuzuia ukatili wa kijinsia.
Tathmini hiyo ilichambua mipango ya kuanzia mwaka wa fedha 2013/14 hadi 2024/25 katika ngazi za kata, shule za msingi na sekondari, pamoja na miundo ya utawala wa jamii.
Matokeo ya tathmini yanaonesha kuwa mipango mingi imejikita zaidi katika maboresho ya miundombinu kama usafishaji na urekebishaji wa mifereji ya maji taka pamoja na usafi wa mazingira.
Hata hivyo, masuala ya haki za afya ya uzazi na ukatili wa kijinsia hayajajumuishwa ipasavyo katika mifumo rasmi ya mipango ya tabianchi.
Aidha, imebainika kuwa ushirikiano kati ya idara za mazingira, afya na jinsia bado ni mdogo, takwimu za kijinsia kuhusu athari za tabianchi hazitoshelezi, na ushiriki wa wanawake, vijana na makundi yaliyotengwa katika maamuzi ya tabianchi ni mdogo.
Kutokana na hali hiyo, tathmini imependekeza kuingizwa kwa viashiria vya haki za afya ya uzazi na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia katika mikakati ya ngazi za mitaa, kuimarisha uratibu wa kisekta, kuweka bajeti za tabianchi zinazozingatia jinsia na kupanua ushiriki wa wanawake na vijana.
Wanafunzi 775 Wawezeshwa Kuwa Mabalozi wa Tabianchi
Mradi huo pia umefikia wanafunzi 775 wenye umri wa miaka 9 hadi 17 kutoka shule 25 kupitia vilabu vya WASH, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuelewa na kushiriki katika masuala ya tabianchi.
Kupitia midahalo, igizo, sanaa na kazi za vikundi, wanafunzi waliwezeshwa kuelewa uhusiano kati ya mabadiliko ya tabianchi, usawa wa kijinsia na haki za afya ya uzazi.
Mbinu hizo shirikishi zimeelezwa kuongeza ushiriki na uhifadhi wa maarifa miongoni mwa wanafunzi.
MyLEGACY imesema kuwa kuwawezesha wanafunzi kuwa “Mabingwa wa Nishati” na mawakala wa mabadiliko kunasaidia kujenga uwajibikaji na kuhamasisha mabadiliko chanya shuleni na katika jamii wanazotoka.
“Mgahawa wa Maarifa”
Waibua Sauti za Jamii
Kupitia jukwaa lake la Mgahawa wa Maarifa, MyLEGACY limefanya midahalo ya kijamii iliyowakutanisha washiriki 249 wakiwemo viongozi wa mitaa, wanawake, vijana, walimu na watu wenye ulemavu.
Majadiliano hayo yamebainisha kuwa jamii zina uelewa wa kina kuhusu changamoto za kimazingira na zina uwezo wa kupendekeza suluhisho endapo zitapatiwa jukwaa salama na jumuishi.
Aidha, imeelezwa kuwa mjadala wa tabianchi unapaswa kuzingatia mwingiliano wa masuala ya kijinsia, ulemavu, elimu na afya, huku kukisisitizwa umuhimu wa kuimarisha mifumo ya utekelezaji ili kuziba pengo kati ya maarifa na vitendo.
Miti 2,000 Yapandwa Mashuleni
Katika hatua za utekelezaji wa vitendo, MyLEGACY imewezesha upandaji wa miti 2,000 ya kivuli na matunda katika shule 24 kupitia vilabu vya WASH na Mazingira. Miti hiyo inatarajiwa kuboresha mazingira ya shule kwa kupunguza joto na vumbi pamoja na kuongeza ustawi wa wanafunzi.
Wanafunzi pia walipata mafunzo ya vitendo kuhusu upandaji na utunzaji wa miti, ikiwemo matumizi ya mifumo rahisi ya umwagiliaji kama drip irrigation kwa kutumia chupa za plastiki zilizotumika.
Shirika hilo limesema kuwa ushirikiano kati ya wanafunzi, walimu, uongozi wa shule na wanajamii umeimarisha uwajibikaji wa pamoja katika uhifadhi wa mazingira na kuhakikisha uendelevu wa hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Kwa ujumla, MyLEGACY imesisitiza kuwa mafanikio ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yanategemea ushirikiano wa sekta zote, hususan vyombo vya habari, katika kuelimisha umma na kusukuma ajenda ya tabianchi inayozingatia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...