NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
Serikali imesema Tanzania inaendelea kupiga hatua kubwa katika ukuaji wa matumizi ya teknolojia, hatua inayochochea maboresho katika sekta mbalimbali ikiwemo utoaji wa huduma za kisheria.
Akifungua mkutano wa siku mbili ulioanza leo Februari 24, 2026 Jijini Dar es Salaam kuhusu Teknolojia na Msaada wa Kisheria uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Zainabu Katimba, alisema kuwa matumizi ya teknolojia si chaguo bali ni hitaji la lazima katika ulimwengu wa sasa.
“Ukuaji wa teknolojia unatoa fursa mpya za kuboresha upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa jamii. Serikali inaangalia kwa makini namna teknolojia itakavyotumika kurahisisha utoaji wa huduma hizo,” alisema Katimba.
Mkutano huo uliwakutanisha wadau wa sheria na teknolojia kutoka nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, ukiwa na lengo la kujadili mbinu bunifu za kutumia teknolojia kuongeza ufanisi na upatikanaji wa haki.
Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo, Mkuu wa Idara za Sheria za Umma kutoka Shule Kuu ya Sheria, Dkt. Boniphace Luhende, akimwakilisha uongozi wa kitaaluma, alisema kuwa kongamano hilo ni jukwaa muhimu la kujifunza na kubadilishana uzoefu.
“Teknolojia ina uwezo mkubwa wa kurahisisha upatikanaji wa haki, hasa kwa wananchi wa maeneo ya mbali. Mkutano huu utasaidia washiriki kuelewa namna bora ya kuitumia,” alieleza.
Kwa upande wake, Dkt. Cecilia Ngaiza kutoka Shule Kuu ya Sheria ya chuo hicho, alisema kuwa majadiliano hayo yatawawezesha washiriki kushirikishana maarifa na uzoefu katika masuala ya kisheria yanayohusiana na teknolojia.
Naye Mhadhiri wa Shule Kuu ya Sheria, Dkt. Petro Protus, alisema lengo kuu la mkutano huo ni kutafuta suluhisho la jinsi wananchi wanavyoweza kupata huduma za kisheria kwa urahisi kupitia mifumo ya kidijitali.
“Tunajadili njia za kuhakikisha teknolojia inakuwa daraja la haki kwa wananchi wote,” alisema.
Wadau wa mkutano huo walisisitiza kuwa matumizi sahihi ya teknolojia katika sekta ya sheria yanaweza kuongeza uwazi, kupunguza gharama na muda wa mashauri, pamoja na kupanua wigo wa msaada wa kisheria kwa wananchi.
Kwa ujumla, ukuaji wa teknolojia katika sekta ya sheria unatarajiwa kurahisisha upatikanaji wa suluhu na haki kwa wananchi kwa wakati na kwa ufanisi zaidi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...