Meneja wa Utahini na Utunuku wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Dkt. Obeid Mahenya akizungumza wakati akifungua mafunzo maalum kwa Maafisa Udahili na Maafisa Mitihani kutoka katika Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini Tanzania katika ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga leo Februari 4,2026
Meneja wa Utahini na Utunuku wa NACTVET, Dkt. Obeid Mahenya akizungumza wakati akifungua mafunzo maalum kwa Maafisa Udahili na Maafisa Mitihani kutoka katika Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini Tanzania


Na Kadama Malunde - Shinyanga


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limeendesha mafunzo maalum kwa Maafisa Udahili na Maafisa Mitihani kutoka katika Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini Tanzania, kwa lengo la kuimarisha ufanisi wa mifumo ya udahili na mitihani katika vyuo hivyo.


Mafunzo hayo ya siku mbili, yanayofanyika Februari 4 na 5, 2026 katika Ukumbi wa NSSF, Manispaa ya Shinyanga, yamewakutanisha maafisa kutoka vyuo mbalimbali nchini kwa ajili ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kutatua changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.


Akifungua kikao kazi hicho kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa NACTVET, Meneja wa Utahini na Utunuku wa Baraza hilo, Dkt. Obeid Mahenya, amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi katika kukuza rasilimali watu wenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira la ndani na kimataifa.


Meneja wa Utahini na Utunuku wa NACTVET, Dkt. Obeid Mahenya.

Ameeleza kuwa sekta hiyo ni mhimili muhimu katika kukuza ajira, kujiajiri, uchumi wa viwanda na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025–2050.

Amesema NACTVET, kama taasisi iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge, Sura ya 129, ina dhamana ya kusimamia na kuhakikisha ubora wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi yanayotolewa nchini ili kuzalisha wahitimu wenye umahiri unaokidhi mahitaji ya soko la ajira.

Hata hivyo, amebainisha kuwepo kwa changamoto mbalimbali, ikiwemo udahili hafifu unaoonekana katika kanzidata ya Baraza pamoja na ucheleweshaji wa upakiaji wa matokeo ya mitihani.

Ametoa mfano kuwa hadi Januari 20, 2026, kulikuwa na chuo kilichosajili wanafunzi wanne pekee katika mfumo wa Baraza kwa mwaka wa masomo 2025/2026, hali isiyoakisi idadi halisi ya wanafunzi waliopo vyuoni.

Kutokana na hali hiyo, NACTVET ililazimika kuongeza muda wa usajili wa wanafunzi hadi Januari 31, 2026 ili kutoa fursa kwa vyuo vyote kusajili wanafunzi katika kanzidata ya Baraza.

Aidha, amesema vyuo vingi vimekuwa vikichelewa au kushindwa kupakia matokeo ya mitihani kwa wakati kulingana na kalenda ya kitaaluma ya Baraza, jambo linaloleta athari kwa wanafunzi na wadau wengine.

Dkt. Mahenya amesisitiza kuwa vyuo vyote vinapaswa kuwasilisha matokeo ya mitihani kupitia kanda husika kabla ya Februari 15, 2026.

Kwa mujibu wa Dkt. Mahenya , changamoto hizo zimekuwa zikisababisha wanafunzi kukosa mikopo ya elimu, kuchelewesha kuendelea na masomo, kuchelewa kwa utoaji wa vyeti pamoja na kukosa fursa za ajira, hali inayokwamisha maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.


Meneja wa NACTVET Kanda ya Kati – Dodoma, Bw. Ramadhani Samainda.


Akizungumza katika kikao kazi hicho, Meneja wa NACTVET Kanda ya Kati – Dodoma, Bw. Ramadhani Samainda, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Udahili, Mitihani na Utunuku wa NACTVET, Dkt. Marcelina Baitilwake, amesema mafunzo hayo yameandaliwa kufuatia changamoto za uelewa mdogo wa mifumo ya udahili na mitihani, kutokuzingatia taratibu na ucheleweshaji wa uthibitishaji wa matokeo, hali inayowaathiri wanafunzi katika kuendelea na masomo, kupata vyeti na fursa za ajira.


Ameeleza kuwa washiriki wanapatiwa mafunzo kuhusu miongozo ya udahili na mitihani, matumizi sahihi ya mifumo ya kielektroniki, ulipaji wa ada za uhakiki wa ubora na upatikanaji wa namba za uthibitisho wa tuzo, kwa lengo la kuongeza ufanisi na ubora wa huduma zinazotolewa vyuoni.


Kupitia mafunzo hayo, amesema Baraza linakusudia kuimarisha uwezo wa maafisa udahili na mitihani, kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao na kuhakikisha huduma zinatolewa kwa wakati kwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.


Amewashauri Maafisa Udahili na Maafisa Mitihani kuhakikisha wanakuwa na Kalenda ya Baraza na kuingiza matukio muhimu katika kalenda za vyuo vyao ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu na kufikia malengo ya pamoja ya Baraza na taasisi zao.

Meneja wa Utahini na Utunuku wa NACTVET, Dkt. Obeid Mahenya akizungumza wakati akifungua mafunzo maalum kwa Maafisa Udahili na Maafisa Mitihani kutoka katika Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini Tanzania

Meneja wa Utahini na Utunuku wa NACTVET, Dkt. Obeid Mahenya akizungumza wakati akifungua mafunzo maalum kwa Maafisa Udahili na Maafisa Mitihani kutoka katika Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini Tanzania

Meneja wa Utahini na Utunuku wa NACTVET, Dkt. Obeid Mahenya akizungumza wakati akifungua mafunzo maalum kwa Maafisa Udahili na Maafisa Mitihani kutoka katika Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini Tanzania

Meneja wa Utahini na Utunuku wa NACTVET, Dkt. Obeid Mahenya akizungumza wakati akifungua mafunzo maalum kwa Maafisa Udahili na Maafisa Mitihani kutoka katika Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini Tanzania

Meneja wa NACTVET Kanda ya Kati – Dodoma, Bw. Ramadhani Samainda, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Udahili, Mitihani na Utunuku wa NACTVET, Dkt. Marcelina Baitilwake kwenye mafunzo maalum kwa Maafisa Udahili na Maafisa Mitihani kutoka katika Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini Tanzania
























Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...