TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Februari 4, 2026, imekutana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule.
Katika mkutano huo wa Tume ulifanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa, Senyamule aliongozana na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.
Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni pamoja na namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pia ushauri wa namna ya kuondokana na matukio hayo.
Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali wakiwemo waathirika wa Matukio hayo ambapo kwa Dodoma tume inaendesha shughuli zake katika Ukumbi wa Takwimu, kwa Mkoa wa Iringa Tume ipo Ukumbi wa Siasa ni Kilimo na kwa Shinyanga Tume ipo katika Ukumbi wa Manisapaa ya Kahama.








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...