Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeibuka mshindi wa kwanza na kutunukiwa tuzo kwa Taasisi zilizofanya vizuri katika uzingatiaji wa Sheria ya Serikali Mtandao, viwango na miongozo kwa taasisi zilizo katika ngazi ya nne ya ukomavu wa TEHAMA Serikalini.

Tuzo hiyo ilitolewa na Ridhiwani Kikwete, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, na kupokelewa na Bw. Donald Mhaiki, Mkurugenzi wa TEHAMA wa NSSF.

Hafla ya utoaji wa tuzo hiyo ilifanyika wakati wa kilele cha Kikao cha 6 cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha International Conference Centre (AICC), jijini Arusha.

Ushindi huo unaonesha jitihada za NSSF katika kuimarisha matumizi ya TEHAMA na kuzingatia kikamilifu sheria, viwango na miongozo ya Serikali Mtandao nchini.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...