Na Diana Byera,Bukoba.

WAKALA wa Nishati Vijijini (REA)umemtambulisha mkandarasi wa kutekeleza Mradi wa umeme katika vitoji 474 vya mkoani Kagera kuanzia Februari 2026 hadi Februari 2029

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Yahaya Ramadhani Kido amepokea timu ya wataalamu kutoka REA ambao waliambatana na mkandarasi anayejulikana CCC International Engineering Nigeria LTD .

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Menaja Miradi Kanda ya Ziwa kwa niaba ya Meneja Mkuu wa REA Ernest Makale amesema Mkoa wa Kagera unavijiji 662 na vyote vimpata umeme.

Pia mkoa huo unavitongoji 3,665 na kati ya hivyo vitongoji 2029 vimepata umeme na vilivyobaki tayari Serikali imeidhinisha vitongoji 474 navyo vinaenda kupata umeme.

Amesema mradi huo utagharimu zaidi ya Sh.bilioni 66.5 na wananchi wa mkoa wa Kagera wapatao 15,396 watanufaika na mradi huo huku mradi wa kusambaza umeme wa vijiji 27 vilivyoko visiwani ukiendelea kukamilika

Ameongeza mradi huo unatarajia kutoa ajira kwa vijana na kuongeza uzoefu kwa vijana ambao wamesomea maswala ya umeme huku akitaka wananchi Kufanya uwekezaji na kujiongozea kipato mara baada ya mradi wa umeme kukamilika

Pia amesema Serikali imefanya mpango wa kuweka Transfoma kubwa katika miradi ya umeme Ili wananchi wanaotaka kufanya uwekezaji Vijijini wafanye shughuli za uwekezaji bila changamoto yeyote.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Wa Kagera Kanali Yahaya Ramadhani Kido ametoa mwito kwa wakandarasi kutekeleza mradi huo kwa Bidiii na kasi kwa sababu mahitaji ya umeme kwa wananchi hasa vitongojini ni makubwa sana.

Amesema pia wakandarasi wanatakiwa kujitambulisha kwa uongozi wa serikali za vijiji ili kupewa ushirikiano na wenyeviti wa vijiji na wananchi wao katika swala la kulinda miundombinu na kutoa maeneo yao ya kupitsha nguzo za umeme.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...