Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU Mkoa wa Lindi, imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 16 baada ya kubaini na kuziba mianya ya ubadhirifu katika miradi ya maendeleo na usimamizi wa rasilimali katika kipindi cha Oktoba hadi Disemba 2025.

Kwa Mujibu wa Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoani humo  EMMA ACKIM MWASOGYE alipokuwa anazungumza na wanahabari mapema leo Februari 27,2026 ,Wilaya ya Ruangwa,uchunguzi uliofanyika kwenye vijiji 15 umeimarisha usimamizi wa misitu na kwamba kamati za misitu zimeundwa na kupewa miongozo, hali iliyosaidia kupunguza uvunaji haramu na kuongeza mapato ya vijiji huku wananchi sasa wakishiriki moja kwa moja kulinda rasilimali zao.

Katika hatua nyingine, amesema Taasisi hiyo katika Wilaya ya Nachingwea ilibaini dosari ujenzi wa Kituo cha Afya Luponda ambapo baadhi ya vifaa vya ujenzi havikuwekwa kwenye makadirio ya gharama na baada  ya ushauri wa taasisi hiyo, marekebisho yalifanyika na mradi unaendelea kwa kuzingatia taratibu.

MWASOGYE amebainisha kuwa TAKUKURU Lindi itaendelea kusimamia kwa karibu miradi ya maendeleo na mifumo ya ukusanyaji mapato ili kuhakikisha fedha za umma zinalindwa na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Amesisitiza kuwa ushirikiano wa wananchi ni muhimu katika kufichua vitendo vya rushwa na ubadhirifu, na kuwataka kuendelea kutoa taarifa.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...