Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi Waziri Salum, ametoa rai kwa watumishi wa wizara na taasisi zinazohusiana na biashara wasiwe vikwazo bali wawewezeshe biashara kuzalishwa kwa wingi.
Aidha, Balozi Salum amewataka wafanyakazi kufanya kazi kwa weledi, utu na bidii, huku akisisitiza umuhimu wa kubadilika ili kufanikisha uwekezaji wa viwanda nchini, kwa kuzingatia maelekezo ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Tusimame pamoja, tufanye kazi, biashara ifanyike, viwanda vijengwe vya kutosha,” alisema Balozi Salum wakati wa ziara yake katika Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) jijini Dar es Salaam.
Alisema pia kwamba wizara inapaswa kutoka kwenye udhibiti na kuelekea kwenye kuwezesha biashara ili Watanzania wanufaike na waweze kutengeneza maendeleo yao. “Serikali kama hatuwezi kuwapa mtaji, tutengeneze mazingira ya unafuu kwa wabunifu,” aliongeza.
Kwa upande wake, Profesa Mkumbukwa Mtambo, Mkurugenzi Mkuu wa TIRDO, amesema amepokea maelekezo hayo na kwamba shirika litahakikisha wananchi, hususan vijana wabunifu, wanafahamu shughuli zinazofanyika ndani ya TIRDO na kushirikishwa katika ubunifu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...